Biblia inasema nini kuhusu Sheria – Mistari yote ya Biblia kuhusu Sheria

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sheria

Kutoka 12 : 14
14 ① Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa BWANA; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele

Kutoka 12 : 24
24 Nanyi mtalitunza jambo hili kuwa ni amri kwako na kwa wanao milele.

Kutoka 12 : 43
43 BWANA akawaambia Musa na Haruni, Amri ya Pasaka ni hii; mtu mgeni asimle;

Kutoka 13 : 10
10 Kwa hiyo utaitunza amri hii kwa wakati wake mwaka baada ya mwaka.

Kutoka 15 : 25
25 Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawajaribu huko;

Hesabu 9 : 14
14 Na kama mgeni akiketi kati yenu ugenini, naye ataka kuishika Pasaka kwa BWANA; kama hiyo sheria ya Pasaka ilivyo, na kama amri yake ilivyo, ndivyo atakavyofanya; mtakuwa na sheria moja, kwa huyo aliye mgeni, na kwa huyo aliyezaliwa katika nchi.

Hesabu 10 : 8
8 ③ Wana wa Haruni, makuhani, ndio watakaopiga hizo tarumbeta; nazo zitakuwa kwenu ni amri ya milele katika vizazi vyenu vyote.

Hesabu 15 : 15
15 ⑱ Katika huo mkutano, kutakuwa na amri moja kwenu ninyi na kwa mgeni akaaye pamoja nanyi; ni amri ya milele katika vizazi vyenu; kama ninyi mlivyo, na mgeni atakuwa vivyo hivyo mbele za BWANA.

Hesabu 18 : 8
8 Kisha BWANA akamwambia Haruni, Tazama, nimekupa wewe ulinzi wa sadaka zangu za kuinuliwa, maana, vitu vyote vya hao wana wa Israeli vilivyowekwa wakfu; nimekupa wewe na wanao vitu hivyo kwa ajili ya kule kutiwa mafuta kwenu, kuwa haki yenu milele.

Isaya 24 : 5
5 ⑤ Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele.

Malaki 4 : 4
4 ⑫ Ikumbukeni Torati ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu.

Warumi 13 : 2
2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu.

1 Petro 2 : 13
13 ⑫ Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; iwe ni mfalme kama mwenye cheo kikubwa;

Isaya 1 : 17
17 jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.

Wagalatia 5 : 6
6 ② Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutotahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.

Wagalatia 6 : 15
15 Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutotahiriwa, ila kiumbe kipya.

Waefeso 2 : 15
15 ⑪ Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani.

Wakolosai 2 : 14
14 ⑯ akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;

Wakolosai 2 : 23
23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.

Waraka kwa Waebrania 9 : 1
1 Basi hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa kidunia.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *