Biblia inasema nini kuhusu Sheria – Mistari yote ya Biblia kuhusu Sheria

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sheria

Kutoka 12 : 49
49 Sheria ni hiyo moja kwa mtu aliyezaliwa kwenu, na kwa mgeni akaaye kati yenu ugenini.

Mambo ya Walawi 24 : 22
22 ① Mtakuwa na sheria moja tu, kwa huyo aliye mgeni, na kwa mzalia; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Hesabu 9 : 14
14 Na kama mgeni akiketi kati yenu ugenini, naye ataka kuishika Pasaka kwa BWANA; kama hiyo sheria ya Pasaka ilivyo, na kama amri yake ilivyo, ndivyo atakavyofanya; mtakuwa na sheria moja, kwa huyo aliye mgeni, na kwa huyo aliyezaliwa katika nchi.

Hesabu 15 : 15
15 ⑱ Katika huo mkutano, kutakuwa na amri moja kwenu ninyi na kwa mgeni akaaye pamoja nanyi; ni amri ya milele katika vizazi vyenu; kama ninyi mlivyo, na mgeni atakuwa vivyo hivyo mbele za BWANA.

Hesabu 15 : 29
29 Mtakuwa na sheria moja kwa huyo afanyaye neno lolote pasipo kujua, kwa huyo aliyezaliwa kwenu kati ya wana wa Israeli, na kwa mgeni akaaye kati yao.

Wagalatia 3 : 28
28 Hakuna Myahudi wala Mgiriki. Hakuna mtumwa wala huru. Hakuna mwanamume wala mwanamke. Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Kristo Yesu.

Hesabu 15 : 35
35 BWANA akamwambia Musa, Mtu huyo lazima atauawa; mkutano wote watampiga kwa mawe huko nje ya kambi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *