Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Shekania
1 Mambo ya Nyakati 3 : 22
22 Na wana wa Shekania ni hawa; Shemaya, na wana wa Shemaya; Hatushi, na Igali, na Baria, na Nearia, na Shafati, watu sita.
Ezra 8 : 3
3 wa wana wa Paroshi, Zekaria; na pamoja naye wakahesabiwa kwa nasaba wanaume mia moja na hamsini.
Ezra 8 : 5
5 Wa wana wa Zatu, Shekania, mwana wa Yahazieli; na pamoja naye wanaume mia tatu.
Ezra 10 : 2
2 ⑤ Hata Shekania, mwana wa Yehieli, mmoja wa wazawa wa Elamu, akajibu, akamwambia Ezra, Sisi tumemkosea Mungu wetu, nasi tumeoa wanawake wageni wa watu wa nchi hizi; lakini bado kuna tumaini kwa Israeli katika jambo hili.
Nehemia 3 : 29
29 ⑱ Na baada yake akajenga Shemaya, mwana wa Shekania, mlinzi wa lango la mashariki.
Nehemia 6 : 18
18 Kwa maana walikuwa watu wengi katika Yuda waliomwapia, kwa sababu alikuwa mkwewe Shekania, mwana wa Ara; naye Yehohanani mwanawe amemwoa binti Meshulamu, mwana wa Berekia.
Nehemia 12 : 3
3 Shekania, Harimu, Meremothi;
Leave a Reply