Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sharon
1 Mambo ya Nyakati 27 : 29
29 na juu ya mifugo iliyolishwa katika Sharoni alikuwa Shitrai, Msharoni; na juu ya mifugo iliyokuwamo mabondeni alikuwa Shafati mwana wa Adlai;
Wimbo ulio Bora 2 : 1
1 Mimi ni ua la uwandani,[1] Ni fahirisi ya mabondeni.
Isaya 33 : 9
9 Nchi inaomboleza, na kulegea; Lebanoni imetahayarika na kunyauka; Sharoni imekuwa kama jangwa; Bashani na Karmeli zimepukutika majani.
Isaya 35 : 2
2 Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa BWANA, ukuu wa Mungu wetu.
Isaya 65 : 10
10 Na Sharoni itakuwa zizi la makundi ya kondoo, na bonde la Akori mahali pa kulala makundi ya ng’ombe, kwa ajili ya watu wangu walionitafuta.
Matendo 9 : 35
35 Na watu wote waliokaa Lida na Sharoni wakamwona, wakamgeukia Bwana.
1 Mambo ya Nyakati 5 : 16
16 ⑤ Nao wakakaa huko Gileadi, katika Bashani, na katika miji yake, na katika viunga vyote vya Sharoni, hadi mipakani mwake.
Leave a Reply