Shaba

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Shaba

Ezekieli 22 : 20
20 Kama vile watu wakusanyavyo fedha, na shaba, na chuma, na risasi, na bati, katika tanuri, ili kuvifukutia moto na kuviyeyusha; ndivyo nitakavyowakusanya ninyi katika hasira yangu, na ghadhabu yangu, nami nitawalaza huko, na kuwayeyusha.

Ayubu 28 : 2
2 Chuma hufukuliwa katika ardhi, Na shaba huyeyushwa katika mawe.

Kumbukumbu la Torati 8 : 9
9 nchi utakayokula mikate humo, pasina shida, hutapungukiwa na kitu ndani yake; nchi ambayo mawe yake ni chuma, na milima yake mnaweza kuchimba shamba.

Yoshua 22 : 8
8 ⑮ kisha akanena nao, na kuwaambia, Rudini na mali mengi mahemani kwenu, na ng’ombe wengi sana, na fedha, na dhahabu, na shaba, na chuma, na mavazi mengi sana; mgawane na ndugu zenu hizo nyara za adui zenu.

2 Samweli 8 : 8
8 Tena toka Tebhathi na toka Berothai, miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi mno.

Ezekieli 27 : 13
13 Ugiriki na Tubali na Mesheki ndio waliokuwa wachuuzi wako; walitoa wanadamu, na vyombo vya shaba, kwa biashara yako.

1 Wafalme 7 : 47
47 ⑱ Sulemani akaviacha vyombo vyote visipimwe kwa kuwa vilikuwa vingi mno; wala uzito wa shaba haukujulikana.

1 Mambo ya Nyakati 22 : 14
14 Basi sasa, tazama, katika shida yangu, nimeiwekea akiba nyumba ya BWANA, talanta laki moja za dhahabu, na talanta milioni moja za fedha; na shaba na chuma isiyo na uzani; kwa vile zilivyo tele; miti tena na mawe nimeweka akiba, nawe utaweza kuongeza.

Kutoka 38 : 31
31 ④ na vitako vya ua kuuzunguka pande zote, na vitako vya lango la huo ua, na vigingi vyote vya maskani, na vigingi vyote vya huo ua uliozunguka pande zote.

1 Wafalme 7 : 47
47 ⑱ Sulemani akaviacha vyombo vyote visipimwe kwa kuwa vilikuwa vingi mno; wala uzito wa shaba haukujulikana.

Ezra 8 : 27
27 na mabakuli ishirini ya dhahabu, thamani yake darkoni elfu moja; na vyombo viwili vya shaba nzuri iliyong’aa, thamani yake sawa na dhahabu.

1 Mambo ya Nyakati 15 : 19
19 Hivyo hao waimbaji, Hemani, Asafu, na Ethani, wakaagizwa kupiga matoazi yao ya shaba kwa sauti kuu;

1 Wakorintho 13 : 1
1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.

1 Samweli 17 : 6
6 Tena amevaa mabamba ya shaba miguuni mwake, naye alikuwa na mkuki wa shaba kati ya mabega yake.

Waamuzi 16 : 21
21 Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho; wakateremka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.

2 Wafalme 25 : 7
7 ⑧ Wakawaua wana wa Sedekia mbele ya macho yake, wakampofusha macho Sedekia, wakamfunga kwa pingu, wakamchukua mpaka Babeli.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *