Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Seraya
2 Samweli 8 : 17
17 ⑦ na Sadoki, mwana wa Ahitubu, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari walikuwa makuhani; na Shausha mwandishi;
2 Samweli 20 : 25
25 na Shausha mwandishi; na Sadoki na Abiathari walikuwa makuhani.
1 Wafalme 4 : 3
3 ⑩ Elihorefu na Ahiya, wana wa Shausha, waandishi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi mwenye kuandika tarehe;[1]
1 Mambo ya Nyakati 18 : 16
16 Na Sadoki mwana wa Ahitubu, na Ahimeleki mwana wa Abiathari, walikuwa makuhani; na Shausha mwandishi;
2 Wafalme 25 : 18
18 ⑱ Na kamanda wa askari walinzi akamtwaa Seraya, kuhani mkuu, na Sefania, kuhani wa pili, na wale walinzi watu wa mlango;
Ezra 7 : 1
1 ⑤ Ikawa baada ya mambo hayo, wakati wa kutawala kwake Artashasta, mfalme wa Uajemi, Ezra, mwana wa Seraya, mwana wa Azaria, mwana wa Hilkia,
2 Wafalme 25 : 21
21 ⑳ Naye mfalme wa Babeli akawapiga, na kuwaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Hivyo Yuda wakachukuliwa utumwani kutoka nchi yao.
Yeremia 52 : 27
27 ⑮ Naye mfalme wa Babeli akawapiga na kuwaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Ndivyo Yuda alivyochukuliwa utumwani, akatolewa katika nchi yake.
2 Wafalme 25 : 23
23 Kisha, wakuu wote wa majeshi, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemweka Gedalia kuwa mtawala, wakamwendea Gedalia huko Mispa; nao ni hawa, Ishmaeli mwana wa Nethania, na Yohana mwana wa Karea, na Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofa, na Yezania mwana wa Mmaaka, wao na watu wao.
Yeremia 40 : 8
8 ndipo wakamwendea Gedalia huko Mizpa; nao ni hawa, Ishmaeli, mwana wa Nethania, na Yohana na Yonathani, wana wa Karea, na Seraya, mwana wa Tanhumethi, na wana wa Efai, Mnetofa, na Yezania, mwana wa Mmaaka, wao na watu wao.
1 Mambo ya Nyakati 4 : 14
14 Na Meonothai akamzaa Ofra; na Seraya akamzaa Yoabu, babaye Ge-harashimu;[3] kwani hao walikuwa mafundi stadi.
1 Mambo ya Nyakati 4 : 35
35 na Yoeli, na Yehu, mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli;
Ezra 2 : 2
2 ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo hesabu ya watu wa Israeli;
Nehemia 12 : 1
1 ⑧ Basi, hawa ndio makuhani na Walawi waliopanda na Zerubabeli, mwana wa Shealueli, na Yoshua; Seraya, Yeremia, Ezra;
Nehemia 12 : 12
12 Na siku za Yoyakimu wakawako makuhani, wakuu wa mbari za mababa; wa Seraya, Meraya; wa Yeremia, Hanania;
Leave a Reply