Biblia inasema nini kuhusu Sefarvaimu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Sefarvaimu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sefarvaimu

2 Wafalme 17 : 24
24 Naye mfalme wa Ashuru akaleta watu kutoka Babeli, na Kutha, na Ava, na Hamathi, na Sefarvaimu, akawaweka katika miji ya Samaria badala ya wana wa Israeli; wakaumiliki Samaria, wakakaa katika miji yake.

2 Wafalme 17 : 31
31 Waavi wakafanya Nibhazi na Tartaki; nao Wasefarvi wakawaunguza wana wao katika moto kwa Adrameleki na Anameleki, miungu ya Sefarvaimu.

2 Wafalme 18 : 34
34 ⑲ Iko wapi miungu ya Hamathi, na ya Arpadi? Iko wapi miungu ya Sefarvaimu, na ya Hena, na ya Iva? Je! Imeuokoa Samaria na mkono wangu?

2 Wafalme 19 : 13
13 Yuko wapi mfalme wa Hamathi, na mfalme wa Arpadi, na mfalme wa mji wa Sefarvaimu, na wa Hena, na wa Iva?

Isaya 36 : 19
19 Wako wapi miungu ya Hamathi na ya Arpadi? Wako wapi miungu ya Sefarvaimu? Je! Wameiokoa Samaria kutoka kwa mkono wangu?

Isaya 37 : 13
13 ④ Yuko wapi mfalme wa Hamathi, na mfalme wa Arpadi, na mfalme wa mji wa Sefarvaimu, wa Hena, na wa Iva?

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *