Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sedekia
2 Wafalme 24 : 18
18 ③ Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na mmoja katika Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Hamutali, binti Yeremia wa Libna.
1 Mambo ya Nyakati 3 : 15
15 Na wana wa Yosia walikuwa hawa; Yohana mzaliwa wa kwanza, wa pili Yehoyakimu, wa tatu Sedekia, wa nne Shalumu.
2 Mambo ya Nyakati 36 : 10
10 ⑥ Mwaka ulipokwisha, Nebukadneza akatuma wajumbe, akamchukua mpaka Babeli; pamoja na vyombo vya thamani vya nyumba ya BWANA; akamtawaza Sedekia nduguye awe mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu.
Yeremia 37 : 1
1 Na Sedekia, mwana wa Yosia, akamiliki baada ya Konia, mwana wa Yehoyakimu, ambaye Nebukadneza amemfanya mtawala katika nchi ya Yuda.
2 Wafalme 24 : 20
20 ④ Maana kwa sababu ya hasira ya BWANA mambo hayo yalitokea katika Yerusalemu na katika Yuda, hata alipokuwa amewaondosha wasiwe mbele ya uso wake; naye Sedekia akamwasi mfalme wa Babeli.
2 Mambo ya Nyakati 36 : 13
13 ⑧ Tena akamwasi mfalme Nebukadneza, aliyemwapisha kwa Mungu; lakini akajifanyia shingo ngumu, akajitia moyo nguvu asimgeukie BWANA, Mungu wa Israeli.
Yeremia 52 : 3
3 Maana, kwa sababu ya hasira ya BWANA, mambo haya yalitokea katika Yerusalemu na katika Yuda, hata akawaondosha wasiwe mbele za uso wake, naye Sedekia akamwasi mfalme wa Babeli.
Ezekieli 17 : 21
21 Na wakimbizi wake wote wa vikosi vyake vyote wataanguka kwa upanga, na hao watakaosalia watatawanyika kwenye kila upepo; nanyi mtajua ya kuwa mimi, BWANA, nimenena neno hili.
Ezekieli 17 : 18
18 Kwa maana amekidharau kiapo kwa kulivunja agano; na tazama, ametia mkono wake, na pamoja na hayo ameyatenda mambo hayo yote; hataokoka.
2 Mambo ya Nyakati 36 : 12
12 akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, Mungu wake; wala hakujinyenyekeza mbele ya Yeremia nabii aliponena kwa kinywa cha BWANA.
Yeremia 21 : 14
14 ⑭ Nami nitawaadhibu kwa kadiri ya matendo yenu, asema BWANA; nami nitawasha moto katika msitu wake, nao utateketeza vitu vyote viuzungukavyo.
Yeremia 24 : 10
10 Nami nitatuma upanga, na njaa, na tauni, kati yao, hata watakapopotelea mbali katika nchi niliyowapa, wao na baba zao.
Yeremia 27 : 22
22 Vitachukuliwa mpaka Babeli, navyo vitakaa huko, hata siku ile nitakapovijia, asema BWANA; hapo ndipo nitakapovileta tena, na kuvirudisha mahali hapa.
Yeremia 32 : 5
5 naye atamchukua Sedekia mpaka Babeli, naye atakuwako huko hadi nitakapomjia, asema BWANA; mjapopigana na Wakaldayo hamtafanikiwa.
Yeremia 37 : 10
10 Maana mngelipiga jeshi lote la Wakaldayo wanaopigana nanyi, wakabaki kati yao watu waliojeruhiwa tu, hata hivyo wangeondoka kila mtu katika hema yake, na kuuteketeza mji huu.
Yeremia 37 : 17
17 ndipo Sedekia, mfalme, akatuma watu wamlete; naye mfalme akamwuliza kwa siri ndani ya nyumba yake, akasema, Je! Liko neno lililotoka kwa BWANA? Yeremia akasema, Liko. Akasema pia, Utatiwa katika mikono ya mfalme wa Babeli.
Yeremia 38 : 28
28 ⑳ Basi Yeremia akakaa katika ukumbi wa walinzi hadi siku ile Yerusalemu ulipotwaliwa.
Ezekieli 12 : 16
16 Lakini nitawasaza watu wachache miongoni mwao na kuwaokoa na upanga, na njaa, na tauni ili watangaze habari ya machukizo yao yote, kati ya mataifa huko waendako; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Ezekieli 17 : 21
21 Na wakimbizi wake wote wa vikosi vyake vyote wataanguka kwa upanga, na hao watakaosalia watatawanyika kwenye kila upepo; nanyi mtajua ya kuwa mimi, BWANA, nimenena neno hili.
Leave a Reply