Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sapphire
Ayubu 28 : 6
6 Mawe yake ni mahali zipatikanapo yakuti; Nayo ina mchanga wa dhahabu.
Ayubu 28 : 16
16 Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri, Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti samawi.
Isaya 54 : 11
11 ⑫ Ewe uliyeteswa, uliyerushwa na tufani, usiyetulizwa, tazama, nitaweka mawe yako kwa rangi nzuri, nitaweka misingi yako kwa yakuti samawi.
Ezekieli 28 : 13
13 Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.
Kutoka 28 : 18
18 na safu ya pili itakuwa zumaridi, na yakuti samawi, na almasi;
Ezekieli 1 : 26
26 Na juu ya anga, lililokuwa juu ya vichwa vyao, palikuwa na mfano wa kiti cha enzi, kuonekana kwake kama yakuti samawi; na juu ya mfano huo wa kiti cha enzi, ulikuwako mfano kama kuonekana kwa mfano wa mwanadamu juu yake.
Ufunuo 21 : 19
19 ⑮ Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawati; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi;
Leave a Reply