Biblia inasema nini kuhusu sanaa ya kijeshi – Mistari yote ya Biblia kuhusu sanaa ya kijeshi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia sanaa ya kijeshi

Zaburi 144 : 1
1 ② Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu, Aifundishaye mikono yangu vita, Na vidole vyangu kupigana.

1 Wakorintho 9 : 24 – 27
24 ⑳ Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate.
25 Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo ili wapokee taji liharibikayo; bali sisi tupokee taji lisiloharibika.
26 Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa;
27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiria wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.

Zaburi 18 : 31 – 35
31 Maana ni nani aliye Mungu ila BWANA? Ni nani aliye mwamba ila Mungu wetu?
32 Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu.
33 Miguu yangu anaifanya kuwa ya kulungu, Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.
34 Anaifundisha mikono yangu vita, Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba.
35 Nawe umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa kulia umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *