Biblia inasema nini kuhusu Salamu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Salamu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Salamu

Ayubu 38 : 22
22 Je! Umeziingia ghala za theluji, Au umeziona ghala za mvua ya mawe,

Hagai 2 : 17
17 Niliwapiga kwa ukavu, na ukungu, na mvua ya mawe, katika kazi zote za mikono yenu; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.

Kutoka 9 : 29
29 ③ Musa akamwambia, Mara nitakapotoka mjini nitamwinulia BWANA mikono yangu; na hizo ngurumo zitakoma, wala haitanyesha mvua ya mawe tena; ili upate kujua ya kuwa dunia hii ni ya BWANA.

Zaburi 78 : 48
48 Akaacha ng’ombe zao wapigwe kwa mvua ya mawe, Na makundi yao kwa umeme.

Zaburi 105 : 32
32 ⑭ Badala ya mvua aliwapa mvua ya mawe, Na umeme uliomulika ghafla katika nchi yao.

Yoshua 10 : 11
11 Kisha ikawa, hapo walipokuwa wakikimbia mbele ya Israeli, hapo walipokuwa wakiteremka Beth-horoni, ndipo BWANA alipowatupia mawe makubwa kutoka mbinguni juu yao hadi kufikia Azeka, nao wakafa; hao waliokufa kwa kuuawa na hayo mawe ya barafu walikuwa ni wengi kuliko hao waliouawa na wana wa Israeli kwa upanga.

Isaya 28 : 2
2 Tazama, Bwana ana mmoja aliye hodari, mwenye nguvu; kama dhoruba ya mvua ya mawe, tufani iharibuyo, kama dhoruba ya maji mengi yafurikayo, ndivyo atakavyotupa chini kwa mkono.

Ufunuo 8 : 7
7 Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyochangamana na damu, vikatupwa juu ya nchi; theluthi ya nchi ikateketea, na theluthi ya miti ikateketea, na majani mabichi yote yakateketea.

Ufunuo 11 : 19
19 Kisha hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la Agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua kubwa ya mawe.

Ufunuo 16 : 21
21 ⑮ Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *