Biblia inasema nini kuhusu Saa – Mistari yote ya Biblia kuhusu Saa

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Saa

Yohana 11 : 9
9 ⑧ Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.

Mathayo 20 : 12
12 wakisema, Hao wa mwisho wamefanya kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na joto la mchana kutwa.

Mathayo 27 : 46
46 ⑪ Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?

Matendo 23 : 23
23 Akawaita maofisa wawili, akasema, Wekeni tayari askari mia mbili kwenda Kaisaria, na askari wapanda farasi sabini, na wenye mikuki mia mbili, kabla ya saa tatu usiku.

Ufunuo 8 : 1
1 Na Mwana-kondoo alipofungua mhuri wa saba, kukawa kimya mbinguni kwa muda wa kama nusu saa.

Ufunuo 9 : 15
15 ⑤ Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *