Rehema

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Rehema

2 Samweli 22 : 26
26 ⑥ Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili Kwa mkamilifu utajionesha kuwa mkamilifu;

Zaburi 18 : 25
25 Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili; Kwa mkamilifu utajionesha kuwa mkamilifu;

Zaburi 37 : 26
26 Mchana kutwa hufadhili na kukopesha, Na mzao wake hubarikiwa.

Zaburi 85 : 10
10 ⑳ Fadhili na kweli zitakutana, Haki na amani zitakumbatiana.

Mithali 3 : 4
4 ② Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.

Mithali 11 : 17
17 Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake; Aliye mkali hujisumbua mwili wake.

Mithali 12 : 10
10 Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake; Bali huruma za mtu mwovu ni ukatili.

Mithali 14 : 22
22 Je! Hawakosi wawazao mabaya? Bali fadhili na kweli zina wao wawazao mema.

Mithali 14 : 31
31 Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake; Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu.

Mithali 20 : 28
28 Fadhili na uaminifu humhifadhi mfalme, Na kiti chake cha enzi huthibitishwa kwa fadhili.

Mithali 21 : 21
21 Aandamaye haki na fadhili, Ataona uhai na haki na heshima.

Hosea 4 : 1
1 Lisikieni neno la BWANA, enyi wana wa Israeli; kwa maana BWANA ana shutuma nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi.

Hosea 12 : 6
6 Basi, mrudie Mungu wako; shika fadhili na hukumu; ukamngojee Mungu wako daima.

Mika 6 : 8
8 Ee mwanadamu, yeye amekuonesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!

Mathayo 5 : 7
7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.

Mathayo 23 : 23
23 ⑯ Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa, bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.

Luka 6 : 36
36 Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.

Warumi 12 : 8
8 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; msimamizi, na asimamie kwa bidii; anayerehemu, na arehemu kwa furaha.

Wakolosai 3 : 13
13 mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.

Mwanzo 39 : 23
23 ⑧ Wala mkuu wa gereza hakufuatilia kazi liliyokuwa mikononi mwa Yusufu; kwa kuwa BWANA alikuwa pamoja naye. BWANA akayafanikisha yote aliyoyafanya.

Yoshua 6 : 25
25 ⑩ Lakini Yoshua akamhifadhi Rahabu, yule kahaba, na watu wa nyumba ya baba yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo; naye akakaa kati ya Israeli hata leo; kwa sababu aliwaficha wale wajumbe aliowatuma Yoshua ili kuupeleleza mji wa Yeriko.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *