Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia rehani
Zaburi 73 : 1 – 28
1 Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, Kwa hao walio safi mioyo yao.
2 Nami miguu yangu ilikuwa karibu kupotoka, Hatua zangu zilikuwa karibu kuteleza.
3 Maana niliwaonea wivu wenye kujivuna, Nilipoiona hali ya amani ya wasio haki.
4 Maana hawana maumivu katika kufa kwao, Na miili yao ina nguvu.
5 Hawana taabu kama watu wengine, Wala hawapati mapigo kama wanadamu wenzao.
6 Hivyo kiburi kimekuwa mkufu shingoni mwao, Udhalimu huwavika kama nguo.
7 Macho yao hutokeza kwa kunenepa, Wameipita kadiri ya mawazo ya mioyo yao.
8 Hudhihaki, husimulia mabaya, Husimulia udhalimu kana kwamba wako juu.
9 Wameweka kinywa chao mbinguni, Na ulimi wao hutangatanga duniani.
10 Kwa hiyo watu wake hugeuka huko, Na maji yaliyojaa humezwa nao.
11 Nao husema, Mungu ajuaje? Yako maarifa kwake aliye juu?
12 Fahamu, ndivyo walivyo wasio haki, Na kwa kustarehe sikuzote wamepata mali nyingi.
13 Hakika nimejisafisha moyo wangu bure, Na kunawa mikono yangu nisitende dhambi.
14 Maana mchana kutwa nimepigwa, Na kuadhibiwa kila asubuhi.
15 Kama ningalisema, Nitasimulia kama hayo; Kumbe! Ningaliwadanganya kizazi cha wana wako.
16 Nami nilifikiri jinsi ya kufahamu hayo; Ikawa taabu machoni pangu;
17 Hata nilipoingia katika patakatifu pa Mungu, Nikautafakari mwisho wao.
18 Hakika Wewe huwaweka penye utelezi, Huwaangusha mpaka palipoharibika.
19 Namna gani wameangamizwa punde! Wakafutiliwa mbali kwa vitisho.
20 Ee Bwana, wamekuwa kama ndoto wakati wa kuamka, Uondokapo utaidharau sanamu yao.
21 Moyo wangu ulipoona uchungu, Viuno vyangu viliponichoma,
22 Nilikuwa kama mjinga, sijui neno; Nilikuwa kama mnyama tu mbele zako.
23 Walakini mimi ni pamoja nawe daima, Umenishika mkono wa kulia.
24 Utaniongoza kwa shauri lako, Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu.
25 Ni nani niliye naye mbinguni, Wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe.
26 Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele.
27 Maana wajitengao nawe watapotea; Umewaangamiza wote waliokuacha Wewe.
28 Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu; Nimefanya kimbilio kwa Bwana MUNGU, Niyahubiri matendo yako yote.
1 Timotheo 5 : 8
8 Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.
Wafilipi 4 : 19
19 Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.
Mithali 28 : 22
22 Mwenye husuda afanya haraka kuwa tajiri; Wala haufikiri uhitaji utakaomjia.
Leave a Reply