Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Refaimu
Mwanzo 14 : 5
5 Na mwaka wa kumi na nne akaja Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja naye, wakawapiga Warefai katika Ashteroth-karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, na Waemi katika Shawe-kiryathaimu,
Mwanzo 15 : 20
20 na Mhiti, na Mperizi, na Mrefai,
Kumbukumbu la Torati 2 : 11
11 na hawa nao wadhaniwa kuwa Warefai[1] kama Waanaki; lakini Wamoabi huwaita Waemi.
Kumbukumbu la Torati 2 : 20
20 (Nchi hiyo nayo yadhaniwa kuwa ni nchi ya Warefai, hapo kale Warefai walikaa humo; lakini Waamoni huwaita Wazamzumi;
Kumbukumbu la Torati 3 : 11
11 (Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho[2] kingali kiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni dhiraa tisa, na upana wake dhiraa nane, kwa mfano wa mkono wa mtu).
Kumbukumbu la Torati 3 : 13
13 na nchi ya Gileadi iliyobaki, na Bashani yote, maana huo ufalme wa Ogu niliwapa nusu ya kabila la Manase; nchi yote ya Argobu, nayo ndiyo Bashani yote. (Na nchi hii yaitwa nchi ya Warefai.
Yoshua 12 : 4
4 tena mpaka wa Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa wa hayo mabaki ya hao Warefai, aliyekaa Ashtarothi na Edrei,
Yoshua 13 : 12
12 ufalme wote wa Ogu uliokuwa katika Bashani, huyo aliyekuwa akitawala katika Ashtarothi na katika Edrei (huyo alisalia katika mabaki ya wale Warefai); kwa kuwa Musa aliwapiga hao na kuwafukuza.
Yoshua 17 : 15
15 Yoshua akawaambia, Kwa kuwa wewe u taifa kubwa la watu, haya, kwea uende mwituni, ujikatie mahali hapo kwa ajili ya nafsi yako katika nchi ya Waperizi, na ya hao Warefai; maana hiyo nchi ya vilima ya Efraimu ni nyembamba, haikutoshi.
Yoshua 15 : 8
8 kisha mpaka ukaendelea karibu na bonde la mwana wa Hinomu, na kufika ubavuni mwa huyu Myebusi upande wa kusini (ndio Yerusalemu); kisha mpaka ukaendelea hata kilele cha mlima ulio pale mkabala wa bonde la Hinomu upande wa magharibi, lililo pale mwisho wa bonde la Warefai upande wa kaskazini;
Yoshua 18 : 16
16 kisha mpaka uliteremka hadi mwisho wa mlima ulio pale mkabala wa bonde la mwana wa Hinomu, lililo pale katika bonde la Warefai, upande wa kaskazini; nao ukateremkia mpaka bonde la Hinomu, hadi ubavuni mwa Myebusi upande wa kusini, kisha ukateremka hadi Enrogeli,
2 Samweli 5 : 18
18 ⑧ Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kujitawanya bondeni mwa Warefai.
2 Samweli 5 : 22
22 Lakini wakapanda hao Wafilisti tena mara ya pili, wakajitawanya bondeni mwa Warefai.
2 Samweli 23 : 13
13 Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai.
1 Mambo ya Nyakati 11 : 15
15 ⑫ Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka mwambani, wakamwendea Daudi, hadi pango la Adulamu; na jeshi la Wafilisti walikuwa wamefanya kambi bondeni mwa Warefai.
1 Mambo ya Nyakati 14 : 9
9 Basi hao Wafilisti walikuwa wamekuja na kujitawanya katika bonde la Warefai.
Isaya 17 : 5
5 Tena itakuwa kama hapo mvunaji ashikapo mabua ya ngano, na mkono wake ukatapo masuke; tena itakuwa kama hapo mtu aokotapo masuke katika bonde la Warefai.
Leave a Reply