Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Rangi
Ayubu 3 : 5
5 Ishikwe na giza, giza tupu, kuwa yake; Wingu na likae juu yake; Chote kiifanyacho siku kuwa giza na kiitishe.
Ayubu 10 : 22
22 Ni nchi ya giza kuu, kama giza lenyewe lilivyo; Ni nchi ya giza tupu, isiyo na mpango wowote wa mambo, Nchi ambayo nuru yake ni kama giza.
Ayubu 30 : 26
26 ⑱ Hapo nilipotazamia mema, ndipo yakaja mabaya; Nami nilipongojea mwanga, likaja giza.
Zaburi 107 : 11
11 ⑬ Kwa sababu waliyaasi maneno ya Mungu, Wakalidharau shauri lake Aliye Juu.
Zaburi 143 : 3
3 Maana adui ameifuatia nafsi yangu, Ameutupa chini uzima wangu. Amenikalisha mahali penye giza, Kama watu waliokufa zamani.
Isaya 5 : 30
30 Nao watanguruma juu yao siku hiyo Kama ngurumo ya bahari; Na mtu akiitazama nchi, ataona giza na dhiki Nayo nuru imetiwa giza katika mawingu yake.
Isaya 8 : 22
22 nao wataiangalia nchi, na, tazama, shida na giza; hapatakuwa changamko kwa sababu ya dhiki; nao watafukuzwa na kuingia katika giza kubwa.
Isaya 9 : 19
19 Kwa sababu ya hasira ya BWANA wa majeshi nchi hii inateketea kabisa; watu hawa nao ni kama kuni zitiwazo motoni; hapana mtu amhurumiaye ndugu yake.
Isaya 24 : 11
11 Pana kilio katika njia kuu kwa sababu ya divai; furaha yote imetiwa giza, na changamko la nchi limetoweka.
Isaya 50 : 3
3 Mimi nazivika mbingu weusi, nami nafanya nguo ya magunia kuwa kifuniko chao.
Yoeli 2 : 6
6 Mbele yao watu wanahangaika; nyuso zote zimegeuka kuwa nyeupe kwa hofu.
Yoeli 2 : 10
10 Nchi inatetemeka mbele yao; mbingu zinatetemeka; jua na mwezi hutiwa giza, na nyota huacha kuangaza;
Yoeli 3 : 15
15 Jua na mwezi vimetiwa giza, na nyota zimeacha kuangaza.
Amosi 5 : 8
8 ⑭ mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA, ndilo jina lake;
Nahumu 2 : 10
10 Amekuwa utupu, na ukiwa, na uharibifu; hata moyo unayeyuka, na magoti yanagonganagongana; moyoni kote mna uchungu, na nyuso za wote zimekuwa nyeupe kwa hofu.
Sefania 1 : 15
15 Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu,
Mathayo 8 : 12
12 bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Mathayo 22 : 13
13 Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Mathayo 25 : 30
30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
2 Petro 2 : 4
4 Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;
Ufunuo 16 : 10
10 ③ Na huyo wa tano akalimimina bakuli lake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama; ufalme wake ukatiwa giza; wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu,
Kutoka 24 : 10
10 ⑱ wakamwona Mungu wa Israeli; chini ya miguu yake palikuwa na kama sakafu iliyofanyizwa kwa yakuti samawi, kama zile mbingu zenyewe kwa usafi wake.
Yeremia 10 : 9
9 Iko fedha iliyofuliwa ikawa mabamba, iliyoletwa kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ufazi, kazi ya fundi stadi na ya mikono ya mfua dhahabu; mavazi yao ni rangi ya samawati na urujuani; hayo yote ni kazi ya mafundi wao.
Ezekieli 1 : 26
26 Na juu ya anga, lililokuwa juu ya vichwa vyao, palikuwa na mfano wa kiti cha enzi, kuonekana kwake kama yakuti samawi; na juu ya mfano huo wa kiti cha enzi, ulikuwako mfano kama kuonekana kwa mfano wa mwanadamu juu yake.
Ezekieli 10 : 1
1 Ndipo nikaangalia, na tazama, katika anga lililokuwa juu ya vichwa vya makerubi, kulionekana juu yao kana kwamba ni yakuti samawi, kuonekana kama mfano wa kiti cha enzi.
Leave a Reply