Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ramah
Yoshua 18 : 25
25 na Gibeoni, na Rama, na Beerothi;
Waamuzi 19 : 13
13 Kisha akamwambia mtumishi wake, Haya, tuifikie miji hii mmojawapo nasi tutalala katika Gibea au katika Rama.
1 Wafalme 15 : 22
22 ⑰ Ndipo mfalme Asa akatangaza kwa Yuda pia; asiachiliwe mtu; nao wakayachukua mawe ya Rama na miti yake, aliyoijengea Baasha; naye mfalme Asa akajenga kwa vitu hivyo Geba wa Benyamini na Mispa.
2 Mambo ya Nyakati 16 : 6
6 Ndipo mfalme Asa akawatwaa Yuda wote; nao wakayachukua mawe ya Rama, na miti yake, aliyoijengea Baasha; naye akajenga kwa vitu hivyo Geba na Mispa.
Ezra 2 : 26
26 Watu wa Rama na Geba, mia sita ishirini na mmoja.
Nehemia 7 : 30
30 Watu wa Rama na Geba, mia sita na ishirini na mmoja.
Nehemia 11 : 33
33 Hazori, Rama, Gitaimu;
Yeremia 40 : 1
1 Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, baada ya wakati ule Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, alipomwacha aende zake toka Rama, baada ya kumchukua akiwa amefungwa minyororo, pamoja na wafungwa wote wa Yerusalemu na Yuda, waliochukuliwa wakiwa wamefungwa mpaka Babeli.
Isaya 10 : 29
29 wamevuka kivuko; wamekwenda kulala katika Geba; Rama unatetemeka; Gibea wa Sauli umekimbia.
Yeremia 31 : 15
15 BWANA asema hivi, Sauti imesikiwa Rama, kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake; asikubali kufarijiwa kwa watoto wake, kwa kuwa hawako.
Hosea 5 : 8
8 ⑩ Pigeni tarumbeta katika Gibea, na baragumu katika Rama; pazeni sauti ya hofu katika Beth-aveni; nyuma yako, Ee Benyamini!
Mathayo 2 : 18
18 Sauti ilisikiwa Rama, Kilio na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake, Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawapo tena.
Mathayo 2 : 18
18 Sauti ilisikiwa Rama, Kilio na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake, Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawapo tena.
Yoshua 19 : 29
29 ⑯ kisha mpaka ulizunguka kuelekea Rama, na mji wa Tiro ulio na boma; kisha mpaka ulizunguka kuelekea Hosa; na matokeo yake yalikuwa baharini katika nchi ya Akzibu;
Yoshua 19 : 36
36 Adama, Rama Hazori;
Waamuzi 4 : 1 – 232
1 Hata alipokufa Ehudi, wana wa Israeli wakafanya yaliyo maovu tena mbele za macho ya BWANA.
2 BWANA akawauza na kuwatia katika mkono wa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori; na Sisera, aliyekaa katika Haroshethi wa Mataifa, alikuwa kamanda wa jeshi lake.
3 Wana wa Israeli wakamlilia BWANA; kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma mia tisa ya vita;[6] naye akawakandamiza sana wana wa Israeli muda wa miaka ishirini.
4 Basi Debora, nabii mwanamke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule.
5 Naye alikuwa akikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue.
6 Siku moja Debora akatuma mtu akamwita Baraka wa Abinoamu kutoka Kedesh-Naftali, akamwambia, BWANA, Mungu wa Israeli anakuamuru hivi: “Nenda, ukawaogoze watu elfu kumi na wana wa Naftali, na wa wana wa Zabuloni, ili washike doria katika mlima Tabori”.
7 Nami nitakuvutia Sisera, kamanda wa jeshi la Yabini, hadi mto wa Kishoni, pamoja na magari yake, na wingi wa watu wake; nami nitamtia mkononi mwako.
8 Baraka akamwambia, Kama utakwenda pamoja nami ndipo nitakwenda; bali kama huendi pamoja nami, mimi siendi.
9 Basi akasema, Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini safari utakayoiendea haitakupatia heshima wewe; maana BWANA atamwuza Sisera katika mkono wa mwanamke. Debora akainuka, akaenda pamoja na Baraka mpaka Kedeshi.
10 Baraka akawakutanisha Naftali na Zabuloni waende Kedeshi wakakwea watu elfu kumi wakimfuata; Debora naye akaenda pamoja naye.
11 Basi Heberi, Mkeni,[7] alikuwa amejitenga na Wakeni, yaani na wana wa Hobabu, shemeji yake Musa, akaipiga hema yake mbali penye mwaloni ulioko Saananimu, karibu na Kedeshi.
12 Watu wakamwambia Sisera ya kwamba Baraka, mwana wa Abinoamu amekwea kwenda mlima wa Tabori.
13 Sisera akayakusanya magari yake yote, naam, magari ya chuma mia tisa, na watu wote waliokuwa pamoja naye, toka Haroshethi wa Mataifa mpaka mto wa Kishoni.
14 Debora akamwambia Baraka, Haya! Inuka; maana siku hii ndiyo siku ambayo BWANA amemtia Sisera katika mkono wako. Je! BWANA hakutoka atangulie mbele yako? Basi Baraka akashuka katika mlima wa Tabori, na watu elfu kumi wakamfuata.
15 BWANA akamfadhaisha Sisera na magari yake yote, na jeshi lake lote, kwa makali ya upanga, mbele ya Baraka; basi Sisera akashuka katika gari lake, akakimbia kwa miguu.
16 Lakini Baraka akayafuatia magari, na jeshi, hadi Haroshethi wa Mataifa; na hilo jeshi lote la Sisera likaanguka kwa makali ya upanga; hakusalia hata mtu mmoja.
17 Lakini Sisera akakimbia kwa miguu, akaifikia hema ya Yaeli mkewe Heberi, Mkeni; kwa maana palikuwa na amani kati ya Yabini, mfalme wa Hazori, na nyumba ya Heberi, Mkeni.
18 Yaeli akatoka kwenda kumlaki Sisera, akamwambia, Karibu Bwana wangu, karibu kwangu; usiogope. Akakaribia kwake hemani, naye akamfunika kwa bushuti.
19 Akamwambia, Tafadhali nipe maji kidogo ninywe; maana nina kiu. Akafungua chupa ya maziwa, akampa kunywa, akamfunika.
20 Naye akamwambia, Simama mlangoni pa hema; kisha itakuwa mtu yeyote akija na kukuuliza, akisema, Je! Yupo mtu hapa, basi, mjibu, La, hapana.
21 ① Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akashika nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akamtia kile kigingi katika kipaji chake, nacho kikapenya, hata kuingia mchangani; kwa maana usingizi mzito ulikuwa umemshika; basi akazimia, akafa.
22 Na tazama, Baraka alipokuwa akimfuatia Sisera; Yaeli akatoka ili kumlaki, akamwambia, Njoo, nami nitakuonesha yule mtu unayemtafuta. Basi akamwendea, na tazama, Sisera amelala humo, amekufa, na hicho kigingi kilikuwa kipajini mwake.
23 ② Basi hivyo Mungu akamshinda Yabini, mfalme wa Kanaani mbele ya wana wa Israeli siku hiyo.
24 Mkono wa wana wa Israeli ukazidi kupata nguvu juu ya Yabini, mfalme wa Kanaani, hata walipokuwa wamemwangamiza Yabini, mfalme wa Kanaani.
Leave a Reply