Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ram
Ruthu 4 : 19
19 na Hesroni akamzaa Ramu; na Ramu akamzaa Aminadabu;
1 Mambo ya Nyakati 2 : 10
10 ⑩ Na Ramu akamzaa Aminadabu; na Aminadabu akamzaa Nashoni, mkuu wa wana wa Yuda;
Mathayo 1 : 4
4 Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni;
Luka 3 : 33
33 ⑭ wa Aminadabu, wa Admini, wa Hesroni, wa Peresi, wa Yuda,
1 Mambo ya Nyakati 2 : 25
25 Na wana wa Yerameeli, mzaliwa wa kwanza wa Hesroni, walikuwa Ramu, mzaliwa wa kwanza, na Buna, na Oreni, na Ozemu; kwa Ahiya.
1 Mambo ya Nyakati 2 : 27
27 Na wana wa Ramu, mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli, walikuwa Maasi, na Yamini, na Ekeri.
Ayubu 32 : 2
2 Ndipo zikawaka hasira za huyo Elihu mwana wa Barakeli, Mbuzi, katika jamaa ya Ramu, juu ya Ayubu, kwa sababu alikuwa amejipa haki mwenyewe zaidi ya Mungu.
Kutoka 26 : 14
14 ② Nawe fanya kifuniko cha ile hema, cha ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo.
Kutoka 39 : 34
34 na kifuniko chake cha ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na kifuniko cha ngozi za pomboo, na pazia la sitara;
Danieli 8 : 3
3 Ndipo nikainua macho yangu nikaona, na tazama, mbele ya mto alisimama kondoo dume, mwenye pembe mbili; na pembe zile mbili zilikuwa ndefu; lakini moja ilikuwa ndefu kuliko ya pili, na ile iliyokuwa ndefu zaidi ilizuka mwisho.
Leave a Reply