Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ocd
1 Petro 5 : 7
7 ⑱ huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
Mathayo 6 : 34
34 ⑪ Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Maovu ya siku yanaitosha siku hiyo.
2 Timotheo 1 : 7
7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Zaburi 4 : 8
8 Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, BWANA, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.
Yohana 14 : 27
27 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.
1 Yohana 4 : 1 – 5
1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zipimeni hizo roho, kama zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
2 Katika hili mnamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.
3 Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
4 Ninyi, watoto wadogo, mnatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.
5 Hao ni wa dunia; kwa hiyo wanena ya dunia na dunia huwasikia.
Zaburi 13 : 1 – 6
1 Ee BWANA, utanisahau hadi lini, hata milele? Hadi lini utanificha uso wako?
2 Nitakuwa na wasiwasi rohoni mwangu hadi lini, Nikihuzunika moyoni mchana kutwa? Adui yangu atatukuka juu yangu hadi lini?
3 Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti.
4 Adui yangu asije akasema, Nimemshinda; Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa.
5 Lakini mimi nimezitumainia fadhili zako; Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.
6 Naam, nitamwimbia BWANA, Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.
Wafilipi 4 : 4 – 8
4 Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.
5 Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yuko karibu.
6 Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.
Yohana 3 : 16
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Yakobo 1 : 5 – 8
5 Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
6 Ila na aombe kwa imani, pasipo mashaka yoyote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari linalochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
8 Mtu wa nia mbili husitasita katika njia zake zote.
Warumi 12 : 2
2 Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Waraka kwa Waebrania 13 : 5
5 Msiwe na tabia ya kupenda fedha; muwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kamwe, wala sitakuacha.
Mathayo 11 : 29
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
Zaburi 77 : 1 – 12
1 Nimpazie Mungu sauti yangu, Naam, nimpazie Mungu, naye atanisikia.
2 ⑭ Katika siku ya taabu yangu nilimtafuta Bwana; Mkono wangu ulinyoshwa usiku, bila kulegea; Nafsi yangu ilikataa kufarijika.
3 Nilipotaka kumkumbuka Mungu nilifadhaika; Nilipotaka kutafakari roho yangu ilizimia.
4 Ulizishika kope za macho yangu zisifumbike; Nilitaabika nisiweze kunena.
5 ⑮ Nilifikiri habari za siku za kale, Miaka ya zamani zilizopita.
6 Nanena na moyo wangu usiku, Nawaza moyoni mwangu, Roho yangu naipeleleza.
7 Je! Bwana atatutupa milele na milele? Asiwe na fadhili kwetu kamwe?
8 ⑯ Rehema zake zimekoma hata milele? Ahadi yake imekwisha hata vizazi vyote?
9 ⑰ Mungu amesahau fadhili zake? Amezuia kwa hasira rehema zake?
10 ⑱ Nikasema, Ndio udhaifu wangu huo; Lakini nitaikumbuka miaka ya mkono wa kulia wake Aliye Juu.
11 ⑲ Nitayakumbuka matendo ya BWANA; Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale.
12 Pia nitaitafakari kazi yako yote; Nitaziwaza habari za matendo yako.
Wafilipi 4 : 8
8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.
Leave a Reply