Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Nyati
Ayubu 39 : 12
12 Je! Utamtumaini kwamba ataileta mbegu yako nyumbani. Na kukusanya nafaka ya kiwanja chako cha kupuria?
Kumbukumbu la Torati 33 : 17
17 Mzaliwa wa kwanza wa ng’ombe wake mume, enzi ni yake; Na pembe zake ni pembe za nyati; Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi; Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu, Nao ni maelfu ya Manase.
Zaburi 22 : 21
21 ⑮ Kinywani mwa simba uniokoe; Naam, toka pembe za nyati umenijibu.
Zaburi 92 : 10
10 Bali pembe yangu umeiinua kama pembe ya nyati, Nimepakwa mafuta mabichi.
Hesabu 24 : 8
8 Mungu amemleta kutoka Misri, Ana nguvu mfano wa nguvu za nyati; Atawameza mataifa walio adui zake, Ataivunja mifupa yao vipande vipande. Atawachoma kwa mishale yake.
Ayubu 39 : 11
11 Je! Utamtumaini kwa sababu ana nguvu nyingi? Au, utamwachia yeye kazi yako?
Isaya 34 : 7
7 Na nyati watateremka pamoja nao, na ndama pamoja na mafahali, na nchi yao italewa kwa damu, na mavumbi yake yatanoneshwa kwa shahamu.
Leave a Reply