Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia njiwa
Mathayo 3 : 16 – 17
16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara aliibuka kutoka majini na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, na kutua juu yake;
17 ⑭ na tazama, sauti kutoka mbinguni ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.
Luka 3 : 21 – 22
21 ⑥ Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka;
22 ⑦ Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.
Mwanzo 8 : 11
11 njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelichuma, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi.
Leave a Reply