Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Njaa
Kumbukumbu la Torati 28 : 57
57 ⑧ na juu ya mchanga wake atokaye katikati ya miguu yake, na juu ya wanawe atakaowazaa; kwa kuwa atawala kwa siri, kwa uhitaji wa vitu vyote; katika mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika malango yako.
Isaya 5 : 13
13 ⑲ Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.
Isaya 9 : 21
21 Manase anamla Efraimu, naye Efraimu anamla Manase; nao wawili pamoja watakuwa juu ya Yuda. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
Isaya 17 : 11
11 Katika siku ile ulipopanda, ulifanya kitalu, na wakati wa asubuhi ulizimeesha mbegu zako, lakini mavuno yatatoweka siku ya huzuni, na ya sikitiko la moyo lifishalo.
Yeremia 5 : 17
17 Nao watakula mavuno yako, na mkate wako, ambao iliwapasa wana wako na binti zako kuula; watakula makundi yako ya kondoo na ya ng’ombe; watakula mizabibu yako na mitini yako; wataiharibu miji yako yenye boma, uliyokuwa ukiitumainia, naam, wataiharibu kwa upanga.
Yeremia 14 : 6
6 Na punda mwitu husimama juu ya vilele vya milima, Hutwetea pumzi kama mbwamwitu; Macho yao hayaoni sawasawa, Kwa kuwa hapana majani.
Yeremia 48 : 33
33 ⑥ Furaha na shangwe zimeondoshwa, katika shamba lizaalo sana, na katika nchi ya Moabu; nami nimeikomesha divai katika mashinikizo; hapana mtu atakayekanyaga zabibu kwa shangwe; shangwe ile itakuwa si shangwe.
Maombolezo 1 : 11
11 Watu wake wote hupiga kite, Wanatafuta chakula; Wameyatoa matamanio yao wapate chakula Cha kuihuisha nafsi; Ee BWANA, tazama, uangalie; Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge.
Maombolezo 1 : 19
19 Niliwaita hao walionipenda Lakini walinidanganya; Makuhani wangu na wazee wangu Walifariki mjini; Hapo walipokuwa wakitafuta chakula ili kuzihuisha nafsi zao.
Maombolezo 2 : 22
22 ⑫ Umeziita kama katika siku ya mkutano wa makini; Hofu zangu zije pande zote; Wala hapana hata mmoja aliyepona wala kusalia Katika siku ya hasira ya BWANA; Hao niliowabeba na kuwalea Huyo adui yangu amewakomesha.
Maombolezo 4 : 10
10 ⑭ Mikono ya wanawake wenye huruma Imewatokosa watoto wao wenyewe; Walikuwa ndio chakula chao Katika uharibifu wa binti ya watu wangu.
Yoeli 1 : 20
20 Naam, hata wanyama pori wanakulilia wewe; Kwa maana vijito vya maji vimekauka, Na moto umeyateketeza malisho ya nyikani.
Mambo ya Walawi 26 : 29
29 ② Nanyi mtakula nyama ya miili ya watoto wenu wa kiume, na nyama ya miili ya binti zenu mtaila.
Kumbukumbu la Torati 28 : 24
24 BWANA atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie.
Kumbukumbu la Torati 28 : 42
42 Miti yako yote, na mazao ya nchi yako, nzige watakuwa nayo.
1 Wafalme 17 : 1
1 ① Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama BWANA, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu.
2 Wafalme 8 : 1
1 Basi Elisha alikuwa amemwambia yule mwanamke, ambaye alimfufulia mwanawe, akasema, Ondoka, ukaende wewe na jamaa yako, ukae hali ya kigeni utakakoweza kukaa; kwa sababu BWANA ameiita njaa; nayo itakuja juu ya nchi hii muda wa miaka saba.
1 Mambo ya Nyakati 21 : 12
12 miaka mitatu ya njaa; au miezi mitatu kuangamia mbele ya adui zako, ukipatwa na upanga wa watesi wako; au siku tatu upanga wa BWANA, yaani tauni katika nchi, na malaika wa BWANA akiharibu kati ya mipaka yote ya Israeli. Haya basi ufikiri ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma.
Zaburi 105 : 16
16 ① Akasababisha njaa katika nchi, Akakiharibu chakula chote walichokitegemea.
Zaburi 107 : 34
34 Nchi ya matunda mengi ikawa uwanda wa chumvi, Kwa sababu ya uovu wa wakazi wake.
Isaya 3 : 8
8 Kwa maana Yerusalemu umebomolewa na Yuda wameanguka, kwa sababu ulimi wao na matendo yao ni kinyume cha BWANA, hata wakayachukiza macho ya utukufu wake.
Isaya 14 : 30
30 Nao walio maskini kabisa watakula, Na wahitaji watajilaza salama; Nami nitatia shina lako kwa njaa, Na mabaki yako watauawa.
Yeremia 14 : 9
9 Kwa nini wewe umekuwa kama mtu aliyeshtuka, kama shujaa asiyeweza kuokoa? Lakini wewe, BWANA, u katikati yetu, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache.
Yeremia 14 : 22
22 ② Je! Katika vitu vya ubatili vya mataifa, kiko kitu kiwezacho kuleta mvua? Je! Mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je! Si wewe, Ee BWANA, Mungu wetu? Kwa sababu hiyo tutakungoja; kwa kuwa wewe umevifanya vitu hivi vyote.
Yeremia 29 : 17
17 ⑩ BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitaleta juu yao upanga, na njaa, na tauni, nami nitawafanya kuwa kama tini mbovu, zisizoweza kuliwa, kwa kuwa ni mbovu sana.
Leave a Reply