Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Net
1 Wafalme 7 : 17
17 Kulikuwa na nyavu kama kazi ya kusuka, na masongo ya mikufu, kwa mataji yaliyokuwako juu ya vichwa vya nguzo; saba kwa taji moja, na saba kwa taji la pili.
Zaburi 35 : 8
8 ⑮ Uharibifu na umpate kwa ghafla, Na wavu aliouficha umnase yeye mwenyewe; Kwa uharibifu aanguke ndani yake.
Mithali 1 : 17
17 Kwa kuwa mtego hutegwa bure, Mbele ya macho ya ndege yeyote.
Isaya 51 : 20
20 Wana wako wamezimia, Wamelala penye pembe za njia kuu zote Kama kulungu wavuni; Wamejaa hasira ya BWANA, Lawama ya Mungu wako.
Mathayo 4 : 21
21 Alipoendelea, akaona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, ambao walikuwa katika mashua pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita.
Mathayo 13 : 47
47 ⑩ Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna;
Luka 5 : 4
4 Na alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.
Ayubu 18 : 8
8 Kwani ametupwa katika wavu na miguu yake mwenyewe, Naye huenda juu ya matanzi.
Ayubu 19 : 6
6 ⑤ Jueni basi kuwa Mungu amenipotosha, Na kunizingira kwa wavu wake.
Zaburi 9 : 15
15 Mataifa wamezama katika shimo walilolichimba; Kwa wavu waliouficha imenaswa miguu yao.
Zaburi 10 : 9
9 Huotea faraghani kama simba pangoni, Huotea amkamate mtu mnyonge. Naam, humkamata mtu mnyonge, Na kumkokota akiwa wavuni mwake.
Zaburi 25 : 15
15 Macho yangu humwelekea BWANA daima, Naye atanitoa miguu yangu katika wavu.
Zaburi 31 : 4
4 Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri, Maana Wewe ndiwe ngome yangu.
Zaburi 35 : 8
8 ⑮ Uharibifu na umpate kwa ghafla, Na wavu aliouficha umnase yeye mwenyewe; Kwa uharibifu aanguke ndani yake.
Zaburi 57 : 6
6 Wameweka wavu ili kuninasa miguu; Nimevunjika moyo; Wamechimba shimo njiani mwangu; Lakini wao wenyewe wametumbukia humo!
Zaburi 66 : 11
11 Ulituingiza ndani ya wavu, Na kuweka viunoni mwetu mzigo uliotulemea.
Zaburi 140 : 5
5 Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba; Wametandika wavu kando ya njia; Wameniwekea matanzi.
Zaburi 141 : 10
10 Wabaya na waanguke katika nyavu zao wenyewe, Wakati ninapopita salama.
Mithali 12 : 12
12 Asiye haki hutamani nyavu za wabaya; Bali shina lao wenye haki huleta matunda.
Mithali 29 : 5
5 Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake, Hutandika wavu ili kuitega miguu yake.
Mhubiri 7 : 26
26 Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti; yaani, mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo; yeye ampendezaye Mungu atamponyoka, bali mwenye dhambi atanaswa na yeye.
Mhubiri 9 : 12
12 Maana mwanadamu naye hajui wakati wake; kama samaki wanaokamatwa katika nyavu mbaya, na mfano wa ndege wanaonaswa mtegoni, kadhalika wanadamu hunaswa katika wakati mbaya, unapowaangukia kwa ghafla.
Leave a Reply