Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ndege
Zaburi 104 : 12
12 Kandokando hukaa ndege wa angani; Na kuimba wakiwa katika matawi.
Mathayo 6 : 25 – 34
25 ④ Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?⑤
26 ⑥ Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kuliko hao?
27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti
29 ⑦ nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa katika tanuri, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 ⑧ Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 ⑩ Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 ⑪ Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Maovu ya siku yanaitosha siku hiyo.
Mathayo 6 : 26
26 ⑥ Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kuliko hao?
Isaya 40 : 31
31 bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Mwanzo 1 : 20
20 Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na viumbe vyenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.
Zaburi 50 : 11
11 Nawajua ndege wote wa milima, Na wanyama wote wa mashamba ni wangu.
Luka 12 : 24
24 ① Watafakarini kunguru, ya kwamba hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala uchaga, lakini Mungu huwalisha. Bora ninyi mara nyingi kuliko ndege!
Zaburi 147 : 9
9 Humpa mnyama chakula chake, Wana-kunguru waliao.
Mwanzo 1 : 21
21 Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Mathayo 10 : 29
29 Je! Mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Wala hata mmoja haanguki chini asipojua Baba yenu;
Zaburi 84 : 1 – 4
1 ⑭ Maskani zako zapendeza kama nini, Ee BWANA wa majeshi!
2 Nafsi yangu imezionea shauku nyua za BWANA, Naam, na kuzikondea. Moyo wangu na mwili wangu Vinamlilia Mungu aliye hai.
3 Hata Shomoro ameona nyumba, Na mbayuwayu amejipatia kiota, Alipoweka makinda yake, Kwenye madhabahu zako, Ee BWANA wa majeshi, Mfalme wangu na Mungu wangu.
4 Heri wakaao nyumbani mwako, Wanakuhimidi daima.
Mithali 27 : 8
8 Kama ndege aendaye huku na huko mbali na kitundu chake; Ndivyo alivyo mtu aendaye huku na huko mbali na mahali pake.
Mithali 1 : 17
17 Kwa kuwa mtego hutegwa bure, Mbele ya macho ya ndege yeyote.
Mathayo 10 : 16
16 Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwamwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
Mathayo 3 : 16
16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara aliibuka kutoka majini na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, na kutua juu yake;
Zaburi 8 : 5 – 8
5 Umemfanya mdogo kuliko Mungu; Umemvika taji la utukufu na heshima;
6 ⑲ Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
7 Kondoo, na ng’ombe wote pia; Naam, na wanyama wa porini;
8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.
Zaburi 91 : 1 – 16
1 Aketiye mahali pa siri pake Aliye Juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2 Atasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.
3 Maana Yeye atakuokoa kutoka kwa mtego wa mwindaji, Na katika maradhi mabaya.
4 ⑳ Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5 Hutaogopa hatari za usiku, Wala mshale urukao mchana,
6 Wala mapigo yajayo usiku, Wala maafa yatokeayo adhuhuri,
7 Hata watu elfu wakianguka ubavuni pako. Naam, watu elfu kumi katika mkono wako wa kulia! Wewe hutakaribiwa na maafa.
8 Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki.
9 Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye Juu kuwa makao yako.
10 Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.
11 Kwa kuwa atakuagizia malaika wake Wakulinde katika njia zako zote.
12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
13 Utawakanyaga simba na nyoka, Mwanasimba na joka utawakanyaga kwa miguu.
14 Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.
15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;
16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonesha wokovu wangu.
Zaburi 68 : 13
13 Kwa nini kulala mazizini arukapo hua, Mbawa zake ziking’aa kama fedha Na manyoya yake kama dhahabu?
Zaburi 104 : 17
17 Humo ndege hujenga viota vyao, Korongo, anayo makao katika misonobari.
Zaburi 55 : 6
6 Nikasema, Ningekuwa na mbawa kama njiwa, Ningeruka mbali na kustarehe.
Leave a Reply