Biblia inasema nini kuhusu Nadhiri – Mistari yote ya Biblia kuhusu Nadhiri

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Nadhiri

Mambo ya Walawi 23 : 38
38 zaidi ya hizo Sabato za BWANA, na zaidi ya matoleo yenu, na zaidi ya hizo nadhiri zenu zote, na zaidi ya sadaka zenu za hiari, ambazo mwampa BWANA.

Hesabu 29 : 39
39 Sadaka hizo mtamsogezea BWANA katika sikukuu zenu zilizoamriwa, zaidi ya nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, kuwa sadaka zenu za kuteketezwa, na sadaka zenu za unga, na sadaka zenu za vinywaji, na sadaka zenu za amani.

Mambo ya Walawi 27 : 13
13 Lakini kwamba ataka kumkomboa kweli, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano juu ya hesabu yako.

Mambo ya Walawi 27 : 15
15 Tena mtu huyo aliyeweka nyumba yake iwe wakfu kama akitaka kuikomboa, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano ya hiyo fedha ya hesabu yako, nayo itakuwa mali yake.

Mambo ya Walawi 27 : 25
25 Na hesabu zako zote zitaandamana shekeli ya mahali patakatifu; gera ishirini zitakuwa shekeli moja.

Mambo ya Walawi 7 : 18
18 ⑳ Tena kama nyama yoyote katika hiyo dhabihu yake ya sadaka za amani ikiliwa siku ya tatu, haitakubaliwa, wala haitahesabiwa kwake huyo mwenye kuisongeza; itakuwa ni machukizo, na mtu atakayeila atachukua uovu wake.

Kumbukumbu la Torati 12 : 6
6 pelekeni huko sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe na ya kondoo;

Kumbukumbu la Torati 12 : 11
11 wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa BWANA.

Kumbukumbu la Torati 12 : 18
18 ⑤ lakini hivyo mtakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, wewe, na mwanao wa kiume na wa kike, na mtumwa wako mume na mke, na Mlawi aliye ndani ya malango yako; nawe furahi mbele za BWANA, Mungu wako, katika yote utakayotia mkono wako.

Kumbukumbu la Torati 12 : 26
26 ⑪ Ila vitu vyako vitakatifu ulivyo navyo, na nadhiri zako, uvitwae uende mahali atakapochagua BWANA;

Hesabu 18 : 14
14 Kila kitu kilichowekwa wakfu katika Israeli kitakuwa chako.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *