Biblia inasema nini kuhusu mwezi – Mistari yote ya Biblia kuhusu mwezi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mwezi

Zaburi 89 : 37
37 ④ Kitathibitika milele kama mwezi; Shahidi mwaminifu aliye mbinguni.

Zaburi 8 : 3
3 ⑰ Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha;

Ufunuo 12 : 1
1 Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji la nyota kumi na mbili.

Kumbukumbu la Torati 4 : 19
19 ⑲ tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo BWANA, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote.

Ufunuo 6 : 12
12 ⑬ Nami nikaona, alipoufungua mhuri wa sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *