Biblia inasema nini kuhusu Mwerezi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mwerezi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mwerezi

Isaya 9 : 10
10 Matofali yameanguka, lakini sisi tutajenga kwa mawe yaliyochongwa; mikuyu imekatwa lakini sisi tutaweka mierezi badala yake.

2 Mambo ya Nyakati 1 : 15
15 Mfalme akafanya fedha na dhahabu kuwa kama mawe humo Yerusalemu, na mierezi akaifanya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi.

2 Mambo ya Nyakati 2 : 4
4 Angalia, najenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wangu, ili kumfanyia wakfu, ya kufukizia mbele zake fukizo la manukato, na ya mkate wa wonyesho wa daima, na ya sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na za siku za sabato, na za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoagizwa za BWANA, Mungu wetu. Hili ni agizo la milele kwa Israeli.

1 Wafalme 5 : 10
10 Basi Hiramu akampa Sulemani miti ya mierezi na miti ya miberoshi kadiri alivyotaka.

1 Wafalme 9 : 11
11 (basi Hiramu, mfalme wa Tiro, alikuwa amemletea Sulemani mierezi na miberoshi, na dhahabu, sawasawa na haja zake zote), ndipo mfalme Sulemani akampa Hiramu miji ishirini ya nchi ya Galilaya.

2 Mambo ya Nyakati 2 : 16
16 ① nasi tutakata miti katika Lebanoni, kadiri utakavyohitaji; na kukuletea tukiieleza baharini mpaka Yafa; nawe utaipeleka Yerusalemu.

Ezra 3 : 7
7 ⑥ Tena waliwapa waashi na maseremala fedha; wakawapa watu wa Sidoni, na watu wa Tiro, chakula, na vinywaji, na mafuta, ili walete mierezi kutoka Lebanoni mpaka Yafa kwa njia ya bahari, kwa kadiri walivyopewa ruhusa na Koreshi, mfalme wa Uajemi.

2 Samweli 5 : 11
11 ④ Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na maseremala, na waashi; nao wakamjengea Daudi nyumba.

1 Mambo ya Nyakati 17 : 1
1 ① Ikawa, Daudi alipokuwa akikaa nyumbani mwake, Daudi akamwambia nabii Nathani, Angalia, mimi ninakaa katika nyumba ya mwerezi, bali sanduku la Agano la BWANA linakaa chini ya mapazia.

1 Wafalme 7 : 2
2 Kisha alijenga nyumba ya msitu wa Lebanoni; mikono mia moja urefu wake, na mikono hamsini upana wake, na mikono thelathini kwenda juu kwake, juu ya safu nne za nguzo za mwerezi, na mihimili ya mwerezi juu ya nguzo.

Ezekieli 27 : 5
5 Mbao zako zote wamezifanya kwa misonobari itokayo Seniri; wametwaa mierezi ya Lebanoni ili kukufanyia mlingoti;

Mambo ya Walawi 14 : 4
4 ② ndipo huyo kuhani ataagiza kwamba watwae kwa ajili yake atakayetakaswa ndege wawili walio hai, ambao ni safi, na mti wa mwerezi, na sufu nyekundu, na hisopo;

Mambo ya Walawi 14 : 6
6 kisha huyo ndege aliye hai atamshika, na huo mti wa mwerezi, na hiyo sufu nyekundu, na hisopo, naye atavichovya, pamoja na yule ndege aliye hai, katika damu ya huyo ndege aliyechinjwa juu ya maji ya mtoni;

Mambo ya Walawi 14 : 52
52 naye ataitakasa hiyo nyumba kwa damu ya ndege, na kwa maji ya mtoni, na kwa huyo ndege aliye hai, na kwa mti wa mwerezi, na kwa hisopo, na kwa sufu nyekundu;

Hesabu 19 : 6
6 ④ kisha kuhani atatwaa mti wa mwerezi, na hisopo, na sufu nyekundu, na kuvitupa katika huo moto unaomchoma ng’ombe.

Zaburi 72 : 16
16 Na uwepo wingi wa nafaka Katika ardhi juu ya milima; Matunda yake na yawayewaye kama ilivyo katika milima ya Lebanoni, Na watu wa mjini wasitawi kama majani ya nchi.

Zaburi 92 : 12
12 Mwenye haki atastawi kama mtende, Atakua kama mwerezi wa Lebanoni.

Isaya 2 : 13
13 Na juu ya mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu na kuinuka, na juu ya mialoni yote ya Bashani;

Isaya 14 : 8
8 ⑬ Naam, misonobari inakufurahia, Na mierezi ya Lebanoni, ikisema, Tokea wakati ulipolazwa chini wewe, Hapana mkata miti aliyetujia.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *