Biblia inasema nini kuhusu Mwanakondoo – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mwanakondoo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mwanakondoo

Kutoka 29 : 41
41 Na huyo mwana-kondoo wa pili utamchinja wakati wa jioni, na utamtoa dhabihu pamoja na sadaka ya nafaka na sadaka yake ya kinywaji kama asubuhi, ili itoe harufu nzuri, iwe dhabihu ya kusogeswa kwa Bwana kwa njia ya moto.

Mambo ya Walawi 3 : 7
7 Ikiwa mtu atamtoa mwana-kondoo kama matoleo yake, ndipo atakapomleta mbele za BWANA;

Mambo ya Walawi 4 : 32
32 ⑱ Naye akileta mwana-kondoo kuwa sadaka ya dhambi, ataleta wa kike mkamilifu.

Mambo ya Walawi 5 : 6
6 naye atamletea BWANA sadaka yake ya hatia kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, mwana-kondoo wa kike, au mbuzi mke, kutoka katika kundi lake, kuwa ni sadaka ya dhambi; kisha kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake.

Mambo ya Walawi 22 : 23
23 Ng’ombe, au mwana-kondoo aliye na kitu kilichozidi, au aliyepungukiwa na kitu katika vitu vya mwilini mwake, mna ruhusa kutoa kuwa sadaka ya moyo wa kupenda; lakini kwa ajili ya nadhiri hatakubaliwa.

Mambo ya Walawi 23 : 12
12 Na siku hiyo mtakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana-kondoo wa kiume asiye na dosari wa mwaka wa kwanza, awe sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA.

Hesabu 6 : 12
12 Kisha ataziweka kwa BWANA hizo siku za kujitenga kwake, naye ataleta mwana-kondoo wa kiume wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya hatia; lakini hizo siku za kwanza hazitahesabiwa, kwa kuwa kule kujitenga kwake kulitiwa unajisi.

Hesabu 7 : 15
15 ng’ombe dume mchanga, mmoja na kondoo dume mmoja, na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

Hesabu 7 : 21
21 na ng’ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

Hesabu 28 : 8
8 Na mwana-kondoo wa pili utamsongeza wakati wa jioni; kama ile sadaka ya unga iliyosongezwa asubuhi, na kama sadaka yake ya kinywaji, ndivyo utakavyoisongeza, ni sadaka ya kusongezwa kwa moto, ni harufu ya kupendeza kwa BWANA.

Kutoka 23 : 19
19 ① Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *