Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mtu
Mwanzo 1 : 26
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila kiumbe kitambaacho nchini.
Mithali 20 : 27
27 Pumzi ya mwanadamu ni taa ya BWANA; Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake.
Ayubu 4 : 17
17 Je! Binadamu atakuwa na haki kuliko Mungu? Je! Mtu atakuwa safi kuliko Muumba wake?
Mwanzo 1 : 27
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Zaburi 33 : 13 – 15
13 Toka mbinguni BWANA huchungulia, Huangalia na kuwaona wanadamu wote.
14 Akiwa katika kiti chake cha enzi. Huwaangalia wote wakaao duniani.
15 Yeye aiumbaye mioyo yao wote Na kuziona kazi zao zote.
Zaburi 8 : 6 – 8
6 ⑲ Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
7 Kondoo, na ng’ombe wote pia; Naam, na wanyama wa porini;
8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.
Zaburi 119 : 73
73 ⑯ Mikono yako iliniumba na kunidhibiti, Unifahamishe nikajifunze amri zako.
Zaburi 138 : 8
8 ⑯ BWANA atanitimizia malengo yake kwangu; Ee BWANA, fadhili zako ni za milele; Usiiache kazi ya mikono yako.
Zaburi 144 : 3
3 ③ Ee BWANA, mtu ni kitu gani hata umjali? Na binadamu hata umwangalie?
Zaburi 100 : 3
3 Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
Zaburi 139 : 14
14 Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa njia ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,
Isaya 43 : 7
7 Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya.
Waraka kwa Waebrania 2 : 7
7 Umemfanya mdogo kwa muda kuliko malaika, Umemvika taji la utukufu na heshima, Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;
Leave a Reply