Biblia inasema nini kuhusu Msukumo – Mistari yote ya Biblia kuhusu Msukumo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Msukumo

Kutoka 19 : 6
6 nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli.

Kutoka 25 : 22
22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.

Hesabu 11 : 29
29 Musa akamwambia, Je! Umekuwa na wivu kwa ajili yangu; ingekuwa heri kama watu wote wa BWANA wangekuwa manabii na kama BWANA angewatia roho yake.

Luka 12 : 12
12 kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema.

2 Timotheo 3 : 16
16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *