Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia msingi
Mathayo 7 : 24
24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
1 Wakorintho 3 : 11 – 13
11 ⑳ Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.
12 Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri.
13 Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani.
Luka 6 : 46 – 48
46 Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, lakini hamyatendi nisemayo?
47 Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonesha mfano wake.
48 Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliipiga nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri.
2 Timotheo 2 : 19
19 ① Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye mhuri huu, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila aliitaye jina la Bwana na auache uovu.
Isaya 28 : 16
16 ④ kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka.
Zaburi 11 : 3
3 Kama misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini?
2 Timotheo 3 : 16
16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
Leave a Reply