Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mshale
Mwanzo 21 : 20
20 ⑯ Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.
Mwanzo 27 : 3
3 ⑰ Basi, nakuomba, chukua uta wako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo;
1 Samweli 31 : 3
3 Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya Sauli, na wapiga upinde wakampata; hata akafadhaika sana kwa sababu ya wapiga upinde.
2 Samweli 22 : 15
15 ② Akapiga mishale, akawatawanya; Umeme, naye akawatimua.
1 Wafalme 22 : 34
34 Mtu mmoja akavuta upinde kwa kubahatisha, akampiga mfalme wa Israeli mahali pa kuungana mavazi yake ya chuma; kwa hiyo akamwambia mwendesha gari lake, Geuza mkono wako, unichukue kutoka katika majeshi; kwa kuwa nimejeruhiwa sana.
2 Wafalme 19 : 32
32 Basi BWANA asema hivi katika habari za mfalme wa Ashuru, Yeye hatauingia mji huu, wala hatapiga mshale hapa, wala hatakuja mbele yake kwa ngao, wala hatajenga boma juu yake.
Zaburi 7 : 13
13 Naye amemtengenezea silaha za kuua, Akifanya mishale yake kuwa mipini ya moto.
Isaya 22 : 3
3 Wakuu wako wote wamekimbia pamoja, Wamefungwa wasiutumie upinde. Wote walioonekana wamefungwa pamoja, Wamekimbia mbali sana.
Yeremia 51 : 3
3 Juu yake apindaye upinde, mwenye upinde na apinde upinde wake, na juu yake ajiinuaye katika dirii yake; msiwaachilie vijana wake; liangamizeni jeshi lake lote.
Ezekieli 21 : 21
21 Maana mfalme wa Babeli alisimama penye njia panda, penye kichwa cha njia hizo mbili, ili atumie uganga; aliitikisa mishale huku na huko, akaziuliza terafi, akayatazama maini.
1 Samweli 20 : 42
42 Naye Yonathani akamwambia Daudi, Nenda kwa amani; kwa maana sisi sote wawili tumeapiana kwa jina la BWANA ya kwamba, BWANA atakuwa kati ya mimi na wewe, na kati ya uzao wangu na uzao wako milele. Daudi akaondoka, akaenda zake; Yonathani naye akaenda zake mjini.
2 Wafalme 13 : 19
19 Yule mtu wa Mungu akamkasirikia, akasema, Ingalikupasa kupiga mara tano au mara sita; ndipo ungaliipiga Shamu hata kuiangamiza; bali sasa utaipiga Shamu mara tatu tu.
Hesabu 24 : 8
8 Mungu amemleta kutoka Misri, Ana nguvu mfano wa nguvu za nyati; Atawameza mataifa walio adui zake, Ataivunja mifupa yao vipande vipande. Atawachoma kwa mishale yake.
Kumbukumbu la Torati 32 : 23
23 Nitaweka madhara juu yao chungu chungu; Nitawapiga kwa mishale yangu hata ikaishe;
Kumbukumbu la Torati 32 : 42
42 ⑥ Nitailevya mishale yangu kwa damu, Na upanga wangu utakula nyama; Pamoja na damu ya waliouawa na waliotekwa nyara, Katika vichwa vya wakuu wa adui.
Ayubu 6 : 4
4 ⑯ Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi iko ndani yangu, Na roho yangu inainywa sumu yake; Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.
Zaburi 11 : 2
2 Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta, Wanaitia mishale yao katika upote, Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo.
Zaburi 21 : 12
12 Kwa maana utawatimua utawafanya wakimbie, Kwa upote wa uta wako utazilenga nyuso zao.
Zaburi 38 : 2
2 Kwa maana mishale yako imenichoma, Na mkono wako umenipata.
Zaburi 45 : 5
5 Mishale yako ni mikali, katika mioyo ya adui za mfalme; Watu huanguka chini yako.
Zaburi 57 : 4
4 Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.
Zaburi 58 : 7
7 Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi; Akiielekeza mishale yake, iwe imetiwa ubutu.
Zaburi 91 : 5
5 Hutaogopa hatari za usiku, Wala mshale urukao mchana,
Leave a Reply