Biblia inasema nini kuhusu Mordekai – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mordekai

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mordekai

Esta 2 : 6
6 ambaye alikuwa amechukuliwa mateka kutoka Yerusalemu miongoni mwa wafungwa waliochukuliwa pamoja na Yekonia, mfalme wa Yuda; ambaye Nebukadneza,[3] mfalme wa Babeli, alimchukua.

Esta 2 : 7
7 Naye alikuwa amemlea Hadasa, yaani, Esta, binti wa mjomba wake, kwa kuwa hana baba wala mama. Naye msichana huyu alikuwa wa umbo nzuri na uso mwema; nao walipokufa baba yake na mama yake, yule Mordekai alimtwaa kuwa binti yake.

Esta 2 : 23
23 Na jambo hilo lilipochunguzwa, na hakika ikapatikana, hao wote wawili wakatundikwa juu ya mti. Hayo pia yakaandikwa katika kitabu cha kumbukumbu mbele ya mfalme.

Esta 6 : 11
11 Ndipo Hamani alipoyatwaa mavazi na farasi, akamvika Mordekai yale mavazi, akampandisha juu ya farasi na kumtembeza kupitia njia kuu ya mjini, akapiga mbiu mbele yake, Hivyo ndivyo atakavyofanyiwa mtu yule ambaye mfalme apenda kumheshimu.

Esta 8 : 2
2 Basi mfalme akaivua pete yake, aliyompokonya Hamani, akampa Mordekai. Naye Esta akamweka Mordekai kuwa juu ya mlango wake Hamani.

Esta 8 : 15
15 ② Naye Mordekai akatoka usoni pa mfalme, amevaa mavazi ya kifalme, ya rangi ya samawati na nyeupe, mwenye taji kubwa la dhahabu, na joho la kitani safi na rangi ya zambarau. Mji wa Susa wakapaza sauti, wakashangilia.

Esta 10 : 3
3 Kwa maana Mordekai Myahudi akiwa wa pili wake mfalme Ahasuero, na mkuu wa Wayahudi, amependeza mbele ya jamii ya ndugu zake; ambaye aliwajali watu wake, na kuiangalia hali njema ya wazawa wao wote.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *