Biblia inasema nini kuhusu Mkopeshaji – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mkopeshaji

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mkopeshaji

Kutoka 21 : 6
6 ndipo hapo huyo bwana wake atamleta mbele ya Mungu na kumleta mlangoni, au penye mwimo wa mlango; na bwana wake atalitoboa sikio lake kwa uma; ndipo atamtumikia sikuzote.

Kutoka 22 : 27
27 maana hiyo nguo ni kifuniko chake, hiyo peke yake ni nguo ya ngozi yake; je! Atalalia nini? Itakuwa, hapo atakaponililia mimi, nitasikia; kwa kuwa mimi ni mwenye rehema.

Mambo ya Walawi 25 : 17
17 ⑪ Wala msidanganyane; lakini utamcha Mungu wako; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Mambo ya Walawi 25 : 37
37 Usimpe fedha yako upate riba, wala usimpe vyakula vyako kwa kujitakia faida.

Kumbukumbu la Torati 15 : 3
3 Waweza kumtoza mgeni; lakini kila uwiacho kwa nduguyo mkono wako utamwachilia.

Kumbukumbu la Torati 23 : 20
20 mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako kwa riba; ili BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika yote utiayo mkono wako, katika nchi uingiayo kuimiliki.

Kumbukumbu la Torati 24 : 6
6 ⑤ Mtu awaye yote asitwae jiwe la kusagia, la juu wala la chini, kuwa rehani; kwani hivi ni kutwaa maisha ya mtu kuwa rehani.

Kumbukumbu la Torati 24 : 13
13 ⑪ Sharti umrudishie rehani lichwapo jua, apate kulala na mavazi yake, na kukubarikia; nayo itakuwa ni haki kwako mbele za BWANA, Mungu wako.

Kumbukumbu la Torati 24 : 17
17 ⑮ Usipotoshe hukumu ya mgeni, wala ya yatima; wala usitwae mavazi ya mjane, yawe rehani;

Mathayo 5 : 42
42 Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.

Luka 6 : 34
34 Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu kwao, mwaonesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili warudishiwe vile vile.

2 Wafalme 4 : 1
1 Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha BWANA; na aliyemdai amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa.

Nehemia 5 : 13
13 Tena nikakung’uta nguo yangu, nikasema, Mungu na amkung’ute vivyo hivyo kila mtu nyumbani mwake, na kazini mwake, asiyeitimiza ahadi hiyo; naam, na akung’utwe vivyo hivyo, na kuwa hana kitu. Mkutano wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA. Nao watu wakafanya kama walivyoahidi.

Ayubu 20 : 20
20 ⑮ Kwa sababu hakujua utulivu ndani yake, Hataokoa chochote kutoka hicho alichokifurahia.

Ayubu 22 : 6
6 Kwa kuwa umetwaa dhamana kwa nduguyo bure, Na kuwavua nguo zao walio uchi.

Ayubu 24 : 3
3 ① Huwanyang’anya yatima punda wao, Humtwaa rehani ng’ombe wake mwanamke mjane.

Ayubu 24 : 10
10 Hata wazunguke uchi bila mavazi, Nao wakiwa na njaa huchukua miganda;

Mithali 22 : 27
27 Kama huna kitu cha kulipa; Kwani ukaondolee kitanda chako chini yako?

Mathayo 5 : 26
26 Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hadi utakapolipa senti ya mwisho.

Luka 12 : 59
59 Nakuambia, Hutoki humo kamwe hadi umalize kulipa hata senti ya mwisho.

Mathayo 18 : 35
35 ⑬ Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.

Zaburi 112 : 5
5 ⑱ Heri atendaye fadhili na kukopesha; Atengenezaye mambo yake kwa haki.

Mathayo 18 : 27
27 Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *