Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mke
Ezekieli 24 : 16
16 Mwanadamu, tazama, ninakuondolea kwa pigo moja tunu, mteule wa macho yako; walakini hutaomboleza wala kulia, wala yasichuruzike machozi yako.
Mwanzo 2 : 18
18 BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
Mwanzo 2 : 20
20 Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye.
Zaburi 128 : 3
3 Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Katika nyumba yako. Wanao watakuwa kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako.
Mwanzo 3 : 16
16 ⑲ Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto; hata hivyo, hamu yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Mwanzo 2 : 18
18 BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
Mwanzo 2 : 24
24 ⑤ Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
1 Wakorintho 11 : 12
12 Maana kama mwanamke alitoka katika mwanamume, vile vile mwanamume naye huzaliwa na mwanamke; na vitu vyote asili yake hutoka kwa Mungu. Hukumuni ninyi wenyewe katika nafsi zenu.
Mwanzo 18 : 6
6 Basi Abrahamu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Tayarisha haraka vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate.
Mithali 31 : 27
27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.
Mwanzo 24 : 67
67 Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mama yake.
Mwanzo 29 : 30
30 Ndipo Yakobo[14] akaingia kwa Raheli, akampenda Raheli kuliko Lea, akatumika kwa ajili yake miaka saba mingine.
Mwanzo 29 : 33
33 Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa BWANA amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni.
Mwanzo 31 : 16
16 Maana mali yote ambayo Mungu amemnyang’anya baba yetu, mali hiyo ndiyo yetu na ya wana wetu. Basi, yoyote Mungu aliyokuambia, uyafanye.
Hesabu 5 : 31
31 Na huyo mume atakuwa hana uovu, na mwanamke atauchukua uovu wake.
Mwanzo 39 : 7
7 Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami.
2 Samweli 11 : 5
5 Yule mwanamke akachukua mimba; basi akapeleka habari na kumwambia Daudi, akasema, Ni mja mzito.
Leave a Reply