Biblia inasema nini kuhusu Mkataba – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mkataba

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mkataba

Yoshua 9 : 15
15 ⑯ Naye Yoshua akafanya amani pamoja nao, na kufanya agano nao, ili kwamba waachwe hai; na wakuu wa mkutano wakawaapia.

1 Wafalme 15 : 19
19 Tumepatana mimi nawe, na baba yangu na baba yako; angalia, nimekuletea zawadi, fedha na dhahabu; basi nenda, uyavunje mapatano yako na Baasha mfalme wa Israeli, ili aache mashambulizi juu yangu.

1 Wafalme 9 : 14
14 Hiramu alikuwa amemletea mfalme talanta[19] mia moja na ishirini za dhahabu.

1 Wafalme 20 : 34
34 Na Ben-hadadi akamwambia, Miji ile baba yangu aliyomnyang’anya baba yako nitairudisha; nawe utajifanyia njia huko Dameski, kama baba yangu aliyoifanya huko Samaria. Ahabu akasema, Nami nitakuacha kwa mapatano haya. Akafanya mapatano naye, akamwacha.

Yoshua 9 : 21
21 ⑳ Wakuu waliwaambia, Waacheni wawe hai; basi wakawa wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya mkutano wote; vile vile kama hao wakuu walivyowaambia.

Yoshua 2 : 21
21 Naye akasema, Na iwe hivyo kama yalivyo maneno yenu. Akawatoa, nao wakaenda zao; naye akaifunga ile kamba nyekundu dirishani

1 Wafalme 5 : 12
12 BWANA akampa Sulemani hekima, kama alivyomwahidia. Ikawa amani kati yao Hiramu na Sulemani; wakafanya mikataba kati yao wawili.

Kutoka 34 : 12
12 ⑭ Ujihadhari nafsi yako, usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe mtego katikati yako.

Kutoka 34 : 15
15 ⑰ Usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi, watu wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, na kuitolea sadaka miungu yao; mtu mmoja akakuita, ukaila sadaka yake.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *