Biblia inasema nini kuhusu Mkalimani – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mkalimani

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mkalimani

Mwanzo 40 : 8
8 ⑬ Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Nawaomba mniambie, kufasiri si ni kazi ya Mungu?

Mwanzo 41 : 16
16 Yusufu akamjibu Farao, akisema, Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani.

Danieli 2 : 30
30 Lakini mimi, sikufunuliwa siri hii kwa sababu ya hekima iwayo yote niliyo nayo zaidi ya watu wengine walio hai, bali kusudi mfalme afunuliwe ile tafsiri, nawe upate kujua mawazo ya moyo wako.

Mwanzo 42 : 23
23 Wala hawakujua ya kwamba Yusufu anawasikia, kwa sababu alizungumza nao kupitia kwa mkalimani.

2 Mambo ya Nyakati 32 : 31
31 Lakini kuhusu wajumbe wa wakuu wa Babeli, waliotumwa kwake kuuliza ajabu iliyofanywa katika nchi, Mungu akamwacha, ili amjaribu, ili kwamba ayajue yote yaliyokuwamo moyoni mwake.

Nehemia 8 : 8
8 Nao wakasoma katika kitabu, katika Torati ya Mungu, kwa sauti ya kusikika; wakaeleza maana yake, hata wakayafahamu yaliyosomwa.

Ayubu 33 : 23
23 ④ Lakini akiwapo malaika pamoja naye, Mpatanishi, mmoja katika elfu, Ili kumwonesha binadamu hayo yampasayo;

1 Wakorintho 12 : 10
10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine fasiri za lugha;

1 Wakorintho 12 : 30
30 Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri?

1 Wakorintho 14 : 5
5 Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kutoa unabii, maana yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa.

1 Wakorintho 14 : 13
13 Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri.

1 Wakorintho 14 : 28
28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu.

Ayubu 33 : 23
23 ④ Lakini akiwapo malaika pamoja naye, Mpatanishi, mmoja katika elfu, Ili kumwonesha binadamu hayo yampasayo;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *