Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mjinga
Mithali 18 : 2
2 Mpumbavu hapendezwi na ufahamu; Ila moyo wake udhihirike tu.
Mithali 26 : 19
19 Ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake, Na kusema, Je! Sikufanya mzaha tu?
Mithali 29 : 11
11 Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote; Bali mwenye hekima huizuia na kuituliza.
Mithali 18 : 6
6 Midomo ya mpumbavu huingia katika fitina, Na kinywa chake huita mapigo.
Mithali 1 : 7
7 Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Mithali 29 : 9
9 Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu; Akikasirika au akicheka, pia hapana raha.
Mathayo 5 : 22
22 ⑫ Bali mimi nawaambieni, Kila amkasirikiaye ndugu yake itampasa hukumu; na mtu akimtusi ndugu yake, anastahili kuhukumiwa na baraza; na mtu akimwambia nduguye, Ewe mpumbavu, anastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.
Mithali 28 : 26
26 Mwenye kujitumainia moyo wake ni mjinga; Bali yeye aendaye kwa busara ataokolewa.
Mithali 26 : 3 – 12
3 Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, Na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu.
4 Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Usije ukafanana naye.
5 Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake.
6 Apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavu Hujikata miguu, na kunywa hasara.
7 Miguu yake achechemeaye huwa dhaifu; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu.
8 Kama mfuko wa vito katika chungu ya mawe; Kadhalika mtu amheshimuye mpumbavu.
9 Kama mwiba uingiao katika mkono wa mlevi; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu.
10 Fundi stadi hufanyiza vitu vyote; Bali amwajiriye mpumbavu ni kama awaajiriye watu wapitao.
11 Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake; Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena.
12 Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
Mithali 10 : 23
23 Kwa mpumbavu kutenda maovu ni kama mchezo; Bali mtu mwenye ufahamu ana hekima.
Tito 3 : 1 – 11
1 Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa watawala na wenye mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema;
2 wasimtukane mtu yeyote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakiwa wapole sana kwa watu wote.
3 Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.
4 Lakini wema wake Mungu Mwokozi wetu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa;
5 ① si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa mara ya pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;
6 ② ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu;
7 ③ ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.
8 Ni neno la kuaminiwa; na mambo hayo nataka uyasisitizie sana, ili wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Mambo hayo ni mazuri sana, tena yana manufaa kwa wanadamu.
9 ④ Lakini ujiepushe na mabishano ya kipumbavu, nasaba, magomvi, na mabishano ya sheria. Kwa kuwa hayana manufaa, tena hayafai kitu.
10 ⑤ Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, tengana naye;
11 ⑥ maana unajua ya kuwa mtu kama huyo ni mpotovu na mtenda dhambi, naye amejihukumia hatia yeye mwenyewe.
Mithali 18 : 7
7 Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake, Na midomo yake ni mtego wa nafsi yake.
Mithali 14 : 7 – 9
7 Toka mbele ya uso wa mpumbavu, Maana hutaona kwake midomo ya maarifa.
8 Akili za mwenye busara ni kujua njia yake; Lakini upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.
9 Wapumbavu huidharau hatia; Bali upo upendeleo kwa wenye haki.
Mithali 3 : 35
35 Wenye hekima wataurithi utukufu, Bali kukuzwa kwa wapumbavu ni fedheha.
Mithali 17 : 28
28 Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.
Mithali 12 : 16
16 Ghadhabu ya mpumbavu hujulikana mara; Bali mtu mwerevu husitiri aibu.
Zaburi 14 : 1
1 Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.
Mithali 15 : 20
20 Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mpumbavu humdharau mamaye.
Mithali 15 : 21
21 ② Upumbavu ni furaha kwake aliyepungukiwa na akili; Bali mwenye ufahamu huunyosha mwenendo wake.
Leave a Reply