Mizani

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mizani

Ayubu 31 : 6
6 (Na nipimwe katika mizani iliyo sawasawa, Ili Mungu aujue uelekevu wangu);

Isaya 40 : 12
12 Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiria mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani?

Isaya 40 : 15
15 Tazama, mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, huhesabiwa kuwa kama mavumbi membamba katika mizani; tazama, yeye huvinyanyua visiwa kama ni kitu kidogo sana.

Ezekieli 5 : 1
1 Nawe, mwanadamu, ujipatie upanga mkali, kama wembe wa kinyozi ujipatie, ukaupitishe juu ya kichwa chako na ndevu zako; kisha ujipatie mizani ya kupimia, ukazigawanye nywele hizo.

Isaya 46 : 6
6 Watu wamwagao dhahabu kutoka mfukoni, na kupima fedha katika mizani, huajiri mfua dhahabu, akaifanya mungu; huanguka, naam, huabudu.

Yeremia 32 : 10
10 Nami nikaitia sahihi ile hati, na kuipiga mhuri, nikawaita mashahidi, nikampimia ile fedha katika mizani.

Mambo ya Walawi 19 : 36
36 Mizani ya haki, vipimo vya haki, efa ya haki, hini ya haki, ndivyo mtakavyokuwa navyo. Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri.

Mithali 16 : 11
11 ⑭ Mizani ya haki na vitanga vyake ni vya BWANA; Mawe yote ya mfukoni ni kazi yake.

Ezekieli 45 : 10
10 ⑤ Mtakuwa na mizani ya haki, na efa ya haki, na bathi ya haki.

Hosea 12 : 7
7 Ni mfanya biashara, aliye na mizani ya udanganyifu mkononi mwake; anapenda kudhulumu.

Amosi 8 : 5
5 mkisema, Mwezi mpya utaondoka lini, tupate kuuza nafaka? Na sabato nayo, tupate kuandaa ngano? Mkiipunguza efa na kuiongeza shekeli, mkidanganya watu kwa mizani ya udanganyifu;

Mika 6 : 11
11 ⑱ Je! Naweza kuwa safi nami nina mizani ya udhalimu, na mfuko wa mawe ya kupimia ya udanganyifu?

Mithali 11 : 1
1 Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza.

Mithali 20 : 23
23 Vipimo mbalimbali ni chukizo kwa BWANA; Tena mizani ya hila si njema.

Ayubu 6 : 2
2 Laiti uchungu wangu ungepimwa, Na msiba wangu kutiwa katika mizani pamoja!

Ayubu 31 : 6
6 (Na nipimwe katika mizani iliyo sawasawa, Ili Mungu aujue uelekevu wangu);

Zaburi 62 : 9
9 Hakika binadamu ni ubatili, Na wenye cheo ni uongo, Katika mizani huinuka; Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.

Isaya 40 : 12
12 Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiria mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani?

Danieli 5 : 27
27 TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka.

Ufunuo 6 : 5
5 ⑦ Na alipoufungua mhuri wa tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *