Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mimea
Mithali 15 : 17
17 Chakula cha mboga palipo na upendo; Ni bora kuliko ng’ombe aliyenona pamoja na kuchukiana.
Mwanzo 1 : 29
29 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mmea utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa chakula chenu;
Mwanzo 9 : 3
3 Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapa hivi vyote.
Kutoka 12 : 22
22 Nanyi twaeni tawi la hisopo, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu yeyote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi.
Hesabu 9 : 11
11 mwezi wa pili, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni,[16] wataishika; watamla pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu;
Waraka kwa Waebrania 6 : 7
7 Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao inalimwa, hupokea baraka zitokazo kwa Mungu;
Leave a Reply