Biblia inasema nini kuhusu mikopo – Mistari yote ya Biblia kuhusu mikopo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mikopo

Mithali 22 : 7
7 Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.

Zaburi 37 : 21
21 Asiye haki hukopa wala halipi, Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu.

Warumi 13 : 8
8 ③ Msiwiwe na mtu chochote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.

Mithali 22 : 26 – 27
26 Usiwe mmoja wao wawekao rehani; Au walio wadhamini kwa deni za watu;
27 Kama huna kitu cha kulipa; Kwani ukaondolee kitanda chako chini yako?

1 Timotheo 5 : 8
8 Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.

Mithali 6 : 1 – 5
1 Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa rafiki yako, Ikiwa wewe na mgeni mmepeana mikono,
2 Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,
3 Sasa, mwanangu, fanya hivi ukajiokoe, Kwa kuwa umejitia mkononi mwa jirani yako; Nenda ukanyenyekee, na kumsihi jirani yako.
4 Usiache macho yako kupata usingizi, Wala kope za macho yako kusinzia.
5 Ujiponye kama paa na mkono wa mwindaji, Na kama ndege katika mkono wa mtega mitego.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *