Mikmash

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mikmash

1 Samweli 13 : 5
5 ⑪ Nao Wafilisti wakakusanyika ili wapigane na Waisraeli, magari elfu thelathini, na wapanda farasi elfu sita, na watu kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi wao; wakapanda juu, wakapiga kambi yao katika Mikmashi, upande wa mashariki wa Beth-aveni.

Ezra 2 : 27
27 Watu wa Mikmashi, mia moja ishirini na wawili.

Nehemia 11 : 31
31 Wana wa Benyamini nao walikuwa wakikaa Geba, na Mikmashi, na Aiya, na Betheli na vijiji vyake;

Isaya 10 : 28
28 Amefika Ayathi; amepita kati ya Migroni; ameweka mizigo yake huko Mikmashi;

1 Samweli 13 : 2
2 Naye Sauli alijichagulia watu elfu tatu wa Israeli; ambao katika hao, elfu mbili walikuwa pamoja na Sauli katika Mikmashi, na katika mlima wa Betheli na elfu moja pamoja na Yonathani katika Gibea ya Benyamini; nao wale watu waliosalia akawaruhusu waende kila mtu hemani kwake.

1 Samweli 14 : 31
31 Nao wakawapiga watu miongoni mwa Wafilisti siku ile kutoka Mikmashi mpaka Ayaloni; na hao watu walikuwa wamepungukiwa sana na nguvu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *