Miji

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Miji

Mwanzo 4 : 17
17 Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Henoko; akajenga mji akauita Henoko, kwa jina la mwanawe.

Mwanzo 10 : 12
12 na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa.

Hesabu 32 : 36
36 na, Beth-nimra, na Beth-harani; miji yenye maboma, na mazizi ya kondoo.

Kumbukumbu la Torati 9 : 1
1 Sikiza, Ee Israeli; hivi leo unataka kuvuka Yordani uingie kwa kuwamiliki mataifa yaliyo makubwa, na yenye nguvu kukupita, miji mikubwa iliyojengewa kuta hadi mbinguni,

Yoshua 10 : 20
20 Kisha ikawa, hapo Yoshua, na wana wa Israeli, walipokuwa wamekwisha kuwaua watu wengi mno, hata wakaangamizwa, na hayo mabaki yao yaliyowasalia walipokuwa wamekwisha ingia katika miji yao yenye boma,

Yoshua 14 : 12
12 Basi sasa unipe mlima huu, ambao BWANA alinena habari zake siku hiyo; kwani wewe ulisikia siku hiyo jinsi Waanaki walivyokuwa huko, na miji ilivyokuwa mikubwa yenye boma; yumkini yeye BWANA atakuwa pamoja nami, nami nitawafukuza watoke nje, kama BWANA alivyonena.

2 Mambo ya Nyakati 8 : 5
5 Tena akaujenga Beth-horoni wa juu, na Beth-horoni wa chini, miji yenye boma, yenye kuta, na malango, na makomeo;

2 Mambo ya Nyakati 11 : 12
12 Na ndani ya miji yote mmoja mmoja aliweka ngao na mikuki, akaifanya kuwa na nguvu nyingi mno. Yuda na Benyamini ikawa milki yake.

2 Mambo ya Nyakati 17 : 2
2 ③ Akaweka jeshi katika miji yote yenye maboma ya Yuda, akatia na askari walinzi katika nchi ya Yuda, na katika miji ya Efraimu, aliyoitwaa Asa babaye.

2 Mambo ya Nyakati 17 : 19
19 Hao ndio waliomngojea mfalme, zaidi ya hao mfalme aliowaweka katika miji yenye maboma katika Yuda yote.

2 Mambo ya Nyakati 21 : 3
3 Baba yao akawapa zawadi kubwa, za fedha, za dhahabu, na za tunu, pamoja na miji yenye maboma katika Yuda; lakini ufalme akampa Yehoramu, kwa sababu alikuwa mzaliwa wa kwanza.

Yoshua 10 : 2
2 ndipo wakaogopa mno, kwa sababu Gibeoni ulikuwa ni mji mkubwa, kama ilivyo miji ya kifalme mmojawapo, tena kwa sababu ulikuwa ni mji mkubwa kupita Ai, tena watu wake wote walikuwa ni mashujaa.

1 Samweli 27 : 5
5 Daudi akamwambia Akishi, Sasa kama nimeona kibali machoni pako na nipewe mahali katika miji hii mmojawapo mashambani, nipate kukaa huko; mbona mtumishi wako akae katika mji wa kifalme pamoja na wewe?

2 Samweli 12 : 26
26 ⑩ Yoabu akapigana juu mji wa Waamoni, akautwaa mji wa kifalme.

1 Mambo ya Nyakati 11 : 7
7 ⑦ Basi Daudi akakaa ngomeni; kwa hiyo ukaitwa mji wa Daudi.

Mwanzo 41 : 48
48 Akakusanya chakula chote cha miaka ile saba katika nchi ya Misri. Akaweka chakula katika miji; chakula cha mashamba yaliyouzunguka kila mji, akakiweka ndani yake.

Kutoka 1 : 11
11 Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.

1 Wafalme 9 : 19
19 na miji yote ya hazina iliyokuwa yake Sulemani; na miji ya magari yake, na miji ya watu wake wapandao farasi, na kila alichopenda kujenga Sulemani huko Yerusalemu, na katika Lebanoni, na katika nchi yote ya mamlaka yake.

2 Mambo ya Nyakati 8 : 4
4 Akaujenga Tadmori wa nyikani, na miji yote ya hazina, aliyoijenga katika Hamathi.

2 Mambo ya Nyakati 16 : 4
4 Naye Ben-hadadi akamsikiliza mfalme Asa, akawatuma makamanda wa majeshi yake juu ya miji ya Israeli; wakapiga Iyoni, na Dani, na Abel-maimu, na miji ya hazina yote ya Naftali.

2 Mambo ya Nyakati 17 : 12
12 Ukuu wake Yehoshafati ukazidi sana; akajenga katika Yuda ngome na miji ya hazina.

2 Mambo ya Nyakati 1 : 14
14 Sulemani akakusanya magari na wapandao farasi; naye alikuwa na magari elfu moja na mia nne, na wapandao farasi elfu kumi na mbili, aliowaweka katika miji ya magari, na pamoja na mfalme huko Yerusalemu.

2 Mambo ya Nyakati 8 : 6
6 na Baalathi, na miji yote ya hazina Sulemani aliyokuwa nayo, na miji yote ya magari yake, na miji ya wapanda farasi wake, na ya anasa yote aliyopenda Sulemani kujenga humo Yerusalemu, na katika Lebanoni, na katika nchi yote ya mamlaka yake.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *