Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mfanyakazi
Mambo ya Walawi 19 : 13
13 ⑰ Usimdhulumu jirani yako, wala kumnyang’anya mali yake; ujira wake aliyeajiriwa usikae kwako usiku kucha hadi asubuhi.
Mambo ya Walawi 25 : 6
6 Na hiyo Sabato ya nchi itakuwa chakula kwenu; kwako wewe, na kwa mtumishi wako, na kwa mjakazi wako, na kwa mtumishi aliyeajiriwa, na kwa mgeni wako akaaye pamoja nawe;
Kumbukumbu la Torati 15 : 18
18 ⑪ Wala usione ugumu, utakapomwacha huru kuondoka kwako; kwani amekutumikia miaka sita kwa ujira mara mbili wa mwajiriwa; na BWANA, Mungu wako, atakubarikia kwa yote utakayofanya.
Kumbukumbu la Torati 24 : 15
15 ⑬ mpe ujira wake kwa siku yake, wala jua lisichwe juu yake; kwa maana ni maskini, moyo wake umeutumainia huo; asije akamlilia BWANA juu yako, ikawa ni dhambi kwako.
Mathayo 10 : 10
10 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mfanyakazi astahili posho yake.
Luka 10 : 7
7 Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mfanya kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihamahame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii.
Warumi 4 : 4
4 Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni.
1 Timotheo 5 : 18
18 Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake.
Ayubu 7 : 3
3 Hivyo basi nami nimepewa miezi ya ubatili iwe fungu langu, Nami nimeandikiwa mateso usiku hata usiku.
Ayubu 14 : 1
1 Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.
Ayubu 14 : 6
6 Acha kumwangalia yeye, apate kupumzika, Hata atakapoitimiza siku yake, kama aliyeajiriwa.
Mathayo 20 : 15
15 Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?
Mathayo 21 : 41
41 Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake.
Yohana 10 : 13
13 Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake.
Ruthu 2 : 4
4 Na tazama, Boazi akaja kutoka Bethlehemu na kuwaamkia wavunaji, akasema, BWANA akae nanyi. Nao wakamwitikia, BWANA na akubariki.
Luka 15 : 17
17 Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kubakiza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.
Luka 15 : 19
19 sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.
Mithali 22 : 16
16 Yeye awaoneaye maskini ili kuongeza mapato, Naye ampaye tajiri, hupata hasara.
Malaki 3 : 5
5 Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami sitasita kutoa ushahidi juu ya wachawi; na juu ya wazinzi, na juu ya waapao kwa uongo; juu ya wamwoneao mwajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema BWANA wa majeshi.
Luka 15 : 16
16 ⑰ Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu.
Leave a Reply