Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mfalme
Ezra 7 : 12
12 ⑪ Artashasta, mfalme wa wafalme, kwa Ezra, kuhani, mwandishi wa Torati ya Mungu wa mbinguni, wasalamu; na kadhalika.
Ezekieli 26 : 7
7 Maana Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitamleta Nebukadneza, mfalme wa Babeli, mfalme wa wafalme, juu ya Tiro toka kaskazini, pamoja na farasi, na magari ya vita, na wapanda farasi, na jeshi, na watu wengi.
Danieli 2 : 37
37 Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu;
Kumbukumbu la Torati 17 : 15
15 usiache kumweka yule atakayechaguliwa na BWANA, Mungu wako, awe mfalme juu yako; umweke mmoja katika ndugu zako awe mfalme juu yako; usimtawaze mgeni juu yako, ambaye si ndugu yako.
1 Samweli 9 : 17
17 Hata Samweli alipomwona Sauli, BWANA akamwambia, Huyu ndiye niliyekuambia juu zake; huyu ndiye atakayewamiliki watu wangu.
1 Samweli 16 : 12
12 Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. BWANA akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.
1 Mambo ya Nyakati 22 : 10
10 ⑭ huyo ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya jina langu; naye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa babaye; nami nitakiimarisha milele kiti cha ufalme wake juu ya Israeli.
2 Mambo ya Nyakati 2 : 12
12 Hiramu akasema tena, Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli, aliyezifanya mbingu na nchi, ambaye amempa mfalme Daudi mwana wa hekima, mwenye busara na akili, ili amjengee BWANA nyumba, na kasri kwa ufalme wake.
Mithali 8 : 15
15 Kwa msaada wangu wafalme humiliki, Na wakuu wanahukumu haki.
Danieli 2 : 21
21 Yeye hubadili majira na nyakati; hutengua na kuteua wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa;
Danieli 2 : 37
37 Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu;
Danieli 4 : 17
17 Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye Juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.
Danieli 5 : 20
20 ⑱ Lakini moyo wake ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa ngumu akatenda kwa kiburi, alishushwa katika kiti chake cha enzi, nao wakamwondolea utukufu wake.
Hosea 8 : 4
4 Wamesimamisha wafalme, lakini si kwa shauri langu; wamejifanyia wakuu, lakini nilikuwa sina habari; kwa fedha yao na dhahabu yao wamejifanyia sanamu, kusudi wakatiliwe mbali.
Hosea 13 : 11
11 Nimekupa mfalme katika hasira yangu, nikamwondoa katika ghadhabu yangu.
1 Samweli 10 : 1
1 ③ Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! BWANA hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa BWANA, na kuwaokoa kutoka kwa mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta][8] uwe mkuu juu ya urithi wake.
1 Samweli 16 : 13
13 Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na Roho ya BWANA ikamjia Daudi kwa nguvu kuanzia siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.
2 Samweli 7 : 16
16 Na nyumba yako, na ufalme wako, vitathibitishwa milele mbele yako. Nacho kiti chako kitaimarishwa milele.
1 Wafalme 1 : 30
30 hakika yake nitafanya leo kama vile nilivyokuapia kwa BWANA, Mungu wa Israeli, nikasema, Kwa yakini Sulemani mwanao atamiliki baada yangu, naye ndiye atakayeketi katika kiti changu cha enzi badala yangu.
2 Mambo ya Nyakati 21 : 4
4 ⑯ Basi Yehoramu alipoinuliwa juu ya ufalme wa babaye, na kujiimarisha, akawaua nduguze wote kwa upanga, na baadhi ya wakuu wa Israeli pia.
Zaburi 89 : 37
37 ④ Kitathibitika milele kama mwezi; Shahidi mwaminifu aliye mbinguni.
1 Mambo ya Nyakati 1 : 51
51 ① Akafa Hadadi. Na hawa ndio majumbe wa Edomu; jumbe Timna, na jumbe Alva, na jumbe Yethethi;
Leave a Reply