Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mdudu
Kutoka 16 : 20
20 Lakini hawakumsikiza Musa; wengine miongoni mwao wakakisaza hata asubuhi, nacho kikaingia mabuu na kutoa uvundo; Musa akawakasirikia sana.
Kutoka 16 : 24
24 ⑧ Basi wakakiweka hata asubuhi, kama Musa alivyowaagiza; nacho hakikutoa uvundo wala kuingia mabuu.
Yona 4 : 7
7 Lakini siku ya pili kulipopambazuka, Mungu akatayarisha buu, nalo likautafuna ule mtango, ukakatika.
Matendo 12 : 23
23 Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na wadudu, akatokwa na roho.
Ayubu 25 : 6
6 ⑫ Seuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!
Isaya 41 : 14
14 ④ Usiogope, Yakobo uliye mdudu, nanyi watu wa Israeli; mimi nitakusaidia, asema BWANA, na mkombozi wako ni Mtakatifu wa Israeli.
Isaya 66 : 24
24 ⑬ Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.
Marko 9 : 44
44 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]
Marko 9 : 46
46 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]
Marko 9 : 48
48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.
Leave a Reply