Mchemraba

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mchemraba

Mwanzo 6 : 16
16 Uifanyie safina mwangaza, ukaumalize juu kiasi cha mkono mmoja; ukautie mlango wa safina katika ubavu wake; ukaifanyie dari tatu, ya chini, ya pili, na ya tatu.

Kumbukumbu la Torati 3 : 11
11 (Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho[2] kingali kiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni dhiraa tisa, na upana wake dhiraa nane, kwa mfano wa mkono wa mtu).

Ezekieli 40 : 5
5 ⑭ Na, tazama, kulikuwa na ukuta nje ya nyumba pande zote, na katika mkono wa mtu yule mwanzi wa kupimia, urefu wake dhiraa sita, kila dhiraa, dhiraa na shubiri; basi akaupima upana wa jengo lile, mwanzi mmoja, na urefu wake, mwanzi mmoja.

Ezekieli 43 : 13
13 ⑥ Na vipimo vya madhabahu kwa dhiraa ni hivi; (dhiraa ni dhiraa na shubiri); kitako chake ni dhiraa moja, na upana wake dhiraa moja; na pambizo yake karibu na ncha yake pande zote, shubiri moja; na hiki kitakuwa kitako cha madhabahu.

Ufunuo 21 : 17
17 Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia moja na arubaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, ambacho malaika alitumia.

Mathayo 6 : 27
27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?

Luka 12 : 25
25 Na yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *