Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mbinguni
Kumbukumbu la Torati 26 : 15
15 Uangalie kutoka makazi yako matakatifu mbinguni, uwabarikie watu wako Israeli, na nchi uliyotupa kama ulivyowaapia baba zetu, nchi imiminikayo maziwa na asali.
Zekaria 2 : 13
13 Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele za BWANA; kwa maana ameamka, na kutoka katika maskani yake takatifu.
1 Wafalme 8 : 30
30 Uisikie dua ya mtumwa wako, na ya watu wako Israeli, watakapoomba wakikabili mahali hapa; naam, sikia huko mbinguni, makao yako; nawe usikiapo, samehe.
1 Wafalme 8 : 39
39 basi, usikie huko mbinguni, makao yako, ukasamehe, ukatende, ukampe kila mtu kwa kadiri ya njia zake; wewe ujuaye moyo wake; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu wote);
1 Wafalme 8 : 43
43 ① basi, usikie huko mbinguni, makao yako, ukatende kwa kadiri ya yote atakayokuomba mgeni huyo; ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe kama watu wako Israeli, nao wajue ya kuwa nyumba hii, niliyoijenga, imeitwa kwa jina lako.
1 Wafalme 8 : 49
49 basi, uyasikie maombi yao na dua yao, huko mbinguni, makao yako, ukaitetee haki yao;
2 Mambo ya Nyakati 6 : 18
18 ③ Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; seuze nyumba hii niliyoijenga!
2 Mambo ya Nyakati 6 : 21
21 ⑤ Uyasikie atakayosihi mtumishi wako, na watu wako Israeli, watakapoomba wakikabili mahali hapa; naam, usikie toka makaoni mwako, toka mbinguni, nawe usikiapo, samehe.
2 Mambo ya Nyakati 6 : 27
27 ⑩ basi usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watumishi wako, na ya watu wako Israeli; uwafundishapo njia njema iwapasayo waiendee; ukainyeshee mvua nchi yako, uliyowapa watu wako iwe urithi.
2 Mambo ya Nyakati 6 : 30
30 ⑫ basi usikie huko mbinguni, ukaapo, ukasamehe, ukampatilize kila mtu kwa kadiri ya njia zake zote; wewe umjuaye moyo; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu);
2 Mambo ya Nyakati 6 : 33
33 basi usikie huko mbinguni, toka makaoni mwako, ukatende yote atakayokuomba huyo mgeni; ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe, kama watu wako Israeli, tena wajue ya kuwa nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa jina lako.
2 Mambo ya Nyakati 6 : 35
35 basi uyasikie huko mbinguni wayaombayo, na kusihi, ukaitetee haki yao.
2 Mambo ya Nyakati 6 : 39
39 basi uyasikie toka mbinguni, toka makaoni mwako, wayaombayo, na kusihi, ukaitetee haki yao; ukawasamehe watu wako, waliokosa juu yako.
Yeremia 23 : 24
24 ⑩ Je, mtu yeyote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema BWANA. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema BWANA.
1 Mambo ya Nyakati 16 : 31
31 Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie; Na waseme katika mataifa, BWANA ametamalaki;
1 Mambo ya Nyakati 21 : 26
26 ② Kisha Daudi akamjengea BWANA madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akamlingana BWANA; naye akamwitikia kutoka mbinguni kwa moto juu ya madhabahu hiyo ya sadaka ya kuteketezwa.
2 Mambo ya Nyakati 7 : 14
14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
Nehemia 9 : 27
27 Kwa sababu hiyo ukawatia katika mikono ya adui zao, waliowasumbua; na wakati wa shida yao, walipokulilia, uliwasikia kutoka mbinguni; na kwa wingi wa rehema zako ukawapa waokozi waliowaokoa kutoka mikononi mwa adui zao.
2 Mambo ya Nyakati 2 : 6
6 Lakini ni nani awezaye kumjengea nyumba, ikiwa mbingu hazimtoshi, wala mbingu za mbingu? Nami ni nani basi, hata nimjengee nyumba, isipokuwa kwa ajili ya pahali pa kufukizia mafusho mbele zake?
2 Mambo ya Nyakati 30 : 27
27 Ndipo wakasimama makuhani Walawi, wakawabariki watu; ikasikiwa sauti yao, sala yao ikafika hata makao yake matakatifu, yaani, mbinguni.
Ayubu 22 : 12
12 Je! Mungu hayuko mbinguni juu? Tena tazama umbali wa nyota, jinsi zilivyo juu!
Ayubu 22 : 14
14 Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; Naye yuatembea juu ya kuba ya mbingu.
Zaburi 2 : 4
4 Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka.
Zaburi 11 : 4
4 BWANA yu katika hekalu lake takatifu. BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni, Macho yake yanaangalia; Kope zake zinawapima wanadamu.
Zaburi 20 : 6
6 Sasa najua kuwa BWANA amwokoa masihi[4] wake; Atamjibu toka mbingu zake takatifu, Kwa matendo makuu ya wokovu Ya mkono wake wa kulia.
Zaburi 33 : 13
13 Toka mbinguni BWANA huchungulia, Huangalia na kuwaona wanadamu wote.
Zaburi 102 : 19
19 Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu, Toka mbinguni BWANA ameiangalia nchi,
Zaburi 103 : 19
19 ⑭ BWANA ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, Na ufalme wake unavitawala vitu vyote.
Leave a Reply