Biblia inasema nini kuhusu Mateso – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mateso

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mateso

Mwanzo 3 : 15
15 ⑱ nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.

Zaburi 2 : 5
5 Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake, Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake, akisema:

Zaburi 22 : 2
2 Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu Na wakati wa usiku lakini sipati raha.

Zaburi 22 : 8
8 ⑩ Husema, Umtegemee BWANA; na amponye; Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye.

Zaburi 22 : 21
21 ⑮ Kinywani mwa simba uniokoe; Naam, toka pembe za nyati umenijibu.

Zaburi 69 : 21
21 Wakanipa uchungu kuwa chakula changu; Na nilipokuwa na kiu wakaninywesha siki.

Zaburi 69 : 26
26 Maana wanamwudhi mtu uliyempiga Wewe, Wanazidisha maumivu ya hao uliowatia jeraha.

Zaburi 109 : 25
25 ② Nami nimekuwa wa kudharauliwa na watu, Wanionapo hutikisa vichwa vyao.

Isaya 49 : 7
7 BWANA, mkombozi wa Israeli, Mtakatifu wake, amwambia hivi yeye anayedharauliwa na wanadamu; yeye anayechukiwa na taifa hili; yeye aliye mtumishi wao watawalao; Wafalme wataona, watasimama; wakuu nao watasujudu; kwa sababu ya BWANA aliye mwaminifu, Mtakatifu wa Israeli aliyekuchagua.

Isaya 50 : 6
6 ② Niliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang’oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate.

Isaya 52 : 14
14 Kama vile wengi walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu yeyote, na umbo lake zaidi ya wanadamu),

Isaya 53 : 5
5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

Isaya 53 : 10
10 ② Lakini BWANA aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake;

Mika 5 : 1
1 ③ Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru; watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni mwake kwa fimbo.

Mathayo 2 : 13
13 Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hadi nitakapokuambia; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.

Mathayo 12 : 14
14 ⑥ Lakini wale Mafarisayo wakatoka wakafanya shauri juu yake jinsi ya kumwangamiza.

Mathayo 12 : 24
24 ⑭ Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo.

Marko 3 : 22
22 Nao waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasema, Ana Beelzebuli, na, Kwa mkuu wa pepo huwatoa pepo.

Luka 6 : 11
11 Wakajawa na uchungu, wakashauriana wao kwa wao wamtendeje Yesu.

Luka 11 : 15
15 ⑬ Wengine wao wakasema, Atoa pepo kwa Beelzebuli, mkuu wa pepo.

Mathayo 16 : 1
1 ① Wakamjia Mafarisayo na Masadukayo, wakamjaribu, wakamwomba awaoneshe ishara itokayo mbinguni.②

Mathayo 26 : 4
4 wakafanya shauri pamoja, ili wamkamate Yesu kwa hila na kumwua.

Mathayo 26 : 16
16 Tokea wakati huo akawa akitafuta nafasi apate kumsaliti.

Mathayo 26 : 59
59 Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo juu ya Yesu, wapate kumwua;

Marko 14 : 1
1 Baada ya siku mbili ilikuwa sikukuu ya Pasaka, na mikate isiyochachwa; wakuu wa makuhani na waandishi wakatafuta njia ya kumkamata kwa hila na kumwua.

Marko 14 : 48
48 Yesu akajibu, akawaambia, Je! Mmekuja na panga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang’anyi?

Mathayo 27 : 30
30 ② Kisha wakamtemea mate, wakautwaa ule mwanzi, wakampigapiga kichwani.

Mathayo 27 : 44
44 Pia wale wanyang’anyi waliosulubiwa pamoja naye walimshutumu vile vile.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *