Biblia inasema nini kuhusu Mapenzi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mapenzi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mapenzi

Kumbukumbu la Torati 6 : 5
5 Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.

Marko 12 : 30
30 ⑩ nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.

Zaburi 19 : 10
10 Ni za kutamanika kuliko dhahabu, Kuliko wingi wa dhahabu safi. Nazo ni tamu kuliko asali, Kuliko sega la asali.

Zaburi 119 : 20
20 Roho yangu imepondeka kwa kutamani Hukumu zako kila wakati.

Zaburi 119 : 97
97 Sheria yako naipenda mno ajabu, Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa.

Zaburi 119 : 103
103 Mausia yako ni matamu sana kwangu, Kupita asali kinywani mwangu.

Zaburi 119 : 167
167 Nafsi yangu imezishika shuhuda zako, Nami nazipenda mno.

1 Mambo ya Nyakati 29 : 3
3 ⑲ Nami tena kwa kuwa nimeiwekea nyumba ya Mungu wangu shauku yangu, nami ninayo hazina yangu mwenyewe ya dhahabu na fedha, ninaitoa kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu, zaidi ya hiyo akiba niliyoiwekea tayari nyumba takatifu;

Zaburi 26 : 8
8 BWANA, nimependa makao ya nyumba yako, Na mahali pa maskani ya utukufu wako.

Zaburi 27 : 4
4 Neno moja nimelitaka kwa BWANA, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa BWANA Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa BWANA, Na kutafakari hekaluni mwake.

Zaburi 84 : 2
2 Nafsi yangu imezionea shauku nyua za BWANA, Naam, na kuzikondea. Moyo wangu na mwili wangu Vinamlilia Mungu aliye hai.

Zaburi 16 : 3
3 Nao watakatifu waliopo duniani, ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.

Warumi 12 : 10
10 Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;

2 Wakorintho 7 : 16
16 Nafurahi, kwa sababu katika kila neno nina moyo mkuu kwa ajili yenu.

1 Wathesalonike 2 : 8
8 Hivyo ndivyo nasi tukiwajali kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.

Wakolosai 3 : 2
2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.

Zaburi 69 : 9
9 Maana mvuto wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.

Zaburi 119 : 139
139 Juhudi yangu imeniangamiza, Maana watesi wangu wameyasahau maneno yako.

Wagalatia 4 : 18
18 Navyo ni vizuri kuonewa shauku katika neno jema sikuzote, wala si wakati nikiwapo mimi pamoja nanyi tu.

Mathayo 10 : 37
37 ⑪ Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *